Posts

TENDE

Image
Unafahamu Umuhimu wa Tende Mwilini..? Jibu Liko Hapa..!!! Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipee. Zifuatazo ni faida ya tunda la tende katika mwili wa binadamu. Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo. Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara. Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina. Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa ...

Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa watano wa Magereza

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa watano wa Magereza kuwa Naibu Makamishna  na  wengine 24 kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi  wa Magereza kuanzia tarehe  25 mwezi Mei, 2017. Waliopandishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Uwesu H. Ngarama,  Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon M. D. Nkana, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Jeremiah .M.C. Nkondo,  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Tusekile S. Mwaisabila, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Augustine S. Mboje ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam. Waliopandishwa vyeo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mag...

Magufuli Akataa Kumia Helikopta.......Asema Atatumia Gari ili Azijue Kero za Wananchi

Image
MGOMBEA urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema katika sehemu kubwa ya kampeni yake, atatumia zaidi usafiri wa barabara ili apate fursa ya kuzijua kwa karibu kero za wananchi katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, alifafanua kuwa kwa maeneo mengine yenye ulazima wa kutumia usafiri mbadala, anaweza kufanya hivyo, lakini dhamira yake ni kutumia zaidi barabara. Aidha, amezitaja sifa ya waziri ajaye wa ujenzi, ambaye atarithi wizara aliyoitumikia kwa miaka 15, iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza katika mkutano wake wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa kampeni za chama hicho katika Kijiji cha Mishamo, kilichopo Kilometa 150 kutoka mkoani Katavi, Dk Magufuli alisema amekataa kutumia helikopta katika baadhi ya sehemu atakazofanya ziara, ili kujionea mwenyewe kero ya barabara inayowakabili Watanzania. Moja ya barabara alizoahidi kujenga ni pamoja na kutoka Tabora mpaka Mpanda, ambayo ina kilometa zaidi ya 356 na ya Mpand...

11 Mbaroni kwa Tuhuma za Kuchoma Moto Kituo cha Polisi Morogoro

Image
                       Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo. POLISI mkoani Morogoro wanashikilia watu 11, wakazi wa Kijiji cha Mpofu wilayani Kilombero kwa tuhuma za kuvamia na kuchoma moto kituo kidogo cha polisi na ofisi ya serikali ya kijiji hicho. Watuhumiwa hao ni sehemu ya zaidi ya watu 100 wanaodaiwa kufanya uhalifu huo katika kituo hicho cha polisi Mbingu, katika taarifa ya Mgeta. Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo wakishinikiza polisi wamwachie mtuhumiwa aliyewekwa mahabusu katika kituo hicho, Bashiri Kadugula (25), kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Veronica Chabula (21) ili wamwadhibu. Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema jana kuwa, Kadugula aliwekwa ndani kwa kumkata mkewe kwa panga sehemu mbalimbali za mwili kutokana na wivu wa mapenzi. Alisema katika tukio hilo ni la Agosti 20...

MALAIKA AANGUKA UINGELEZA.

Image
Tukio Lisilo la Kawaida MALAIKA Aanguka Nchini UINGEREZA..Watu Wamiminika Kushuhudia Picha ya karibu ikionesha sura ya malaika huyo na mbawa zake. Tukio lisilo la kawaida limetoa huko Uingereza.... MALAIKA aanguka nchini UINGEREZA na kuifadhiwa sehemu maalum ambapo watu wameanza kumiminika kwenda kumshuhudia Baadhi ya laia waliofika kushuhudia tukio hilo wakiwa hawaamini kilichotokea. Akiwa kahifadhiwa kwenye sehemu maalum,picha ikionesha kwa mbali .

Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo

Image
Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo Sos Mpekuzi blog Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema watu  zaidi  ya 10  wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.   Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma.Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu.

Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa

Image
Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa Ziara ya Obama nchini kenya Shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi. Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa imetua. Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.   ...