Posts

KITUO CHA KUHESABIA KURA CHA MUUNGANO WA UPINZANI KENYA CHAVAMIWA

Image
Ikiwa ni siku chache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Kenya, Muungano wa Upinzani (NASA) umeishutumu serikali kuwa imevamia moja ya vituo vyake vya kuhesabia kura kilichopo eneo la Westlands jijini Nairobi. Msemaji wa NASA ameeleza kuwa wanaume waliokuwa wamefunika nyuso zao walivamia ofisi hiyo wakafanya uharibifu na kubeba kompyuta, simu za mkononi na vitabu. Kwa upande wake, serikali ya nchi hiyo imesisitiza kuwa hakuna uvamizi uliofanyika, . Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa atakubali tu kushindwa ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki. Hivi karibuni, Rais wa Uhuru Kenyatta alikaririwa akisema ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo wa siku ya Jumanne licha ya kila mmoja kusisitiza kuwa ataibuka mshindi. Uchaguzi wa Kenya mara nyingi umekua ukikumbwa na ghasia. Zaidi ya watu 1000 waliuawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. TAGS:

Washukiwa wa Mauaji ya Mkurugenzi TEHAMA Kenya Wakamatwa Uganda.

Image
WASHUKIWA WA MAUAJI YA MKURUGENZI TEHAMA KENYA WAKAMATWA Jeshi la Polisi nchini Uganda linawashikiliwa watuhumiwa 3 (Mkenya 1 na Waganda 2) wa mauaji ya Meneja wa TEHAMA wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, Chris Msando. Msando alitoweka nchini Kenya na kupatikana akiwa amefariki. Polisi wa Uganda wamesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na gari aina ya Toyota Fortuner. Gari hilo lenye namba za usajiri za Uganda huku ikidaiwa lilikuwa na namba za Kenya wakati wa kuvuka mpaka wa Busia. ​ Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi majira ya saa 9 alfajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake. Marekani na Uingereza zilikubali kutoa maofisa wao wawili wa ngazi za juu kutoka mashirika ya upelelezi ya FBI na Scotland Yard baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Keriako Tobiko kutaka uchunguzi ufanywe kuhusu mauaji ya Msando. Aliitaka pia serikali kuhakikisha usalama wa maofisa wa IEBC ili uchaguzi ufanyike kwa usalama. Polisi ...

Rais Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kura nyingi Rwanda

Image
Haki miliki ya picha Image caption Kagame alipiga kura mjini Kigali Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo. Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba. Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa. Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana Haki miliki ya picha Image caption Kutoka kushoto Paul Kagame, Frank Habineza na Philippe Mpayimana Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa. Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadi...

Lowassa Atua Kenya Kumnadi Uhuru Kenyatta

Image
Zikiwa zimebaki siku mbili nchi ya Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amefunguka sababu kuu zinazofanya amtetee na kumnadi mgombea Urais kupitia chama cha Jubilee Uhuru Kenyatta kuwa ni kiongozi shupavu. Lowassa ambaye jana alishiriki katika mkutano wa chama cha Jubilee alisema kuwa kuna watu wanauliza kwanini yeye pamoja na CHADEMA wanamnadi kwa kuwa kiongozi huyo ni shupavu na mpenda watu. "Kuna watu wananiuliza kwanini mnamnadi Uhuru Kenyatta, nasema tena hadharani bila aibu yoyote huyu ni kiongozi shupavu anayependa watu, anaweza kuongoza watu wetu, lakini cha pili Uhuru Kenyatta anapenda Afrika Mashariki akiingia madarakani ataturuhusu tuendelee kuzunguka zunguka kwenye mipaka hii kama Namanga pale bila hata shida, la tatu ni kwamba aliingia madarakani nchi ikiwa kwenye vita lakini amewapa suluhu ameingoza nchi imekwenda taratibu na akafanikiwa"  alisema Lowassa Mbali na hilo Lowassa alisema kuwa licha ya mambo ...

BANGI ZAMPONZA MBUNGE WA CHADEMA

Image
Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche jana alikamatwa na polisi alipokwenda kituo cha polisi cha Tarime kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake. Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba amesema kuwa polisi walimkamata Heche kutokana na kauli zake ikiwepo kauli ya kutaka kilimo cha bangi kihalalishwe pamoja na kauli yake ya kuzuia shughuli za ACACIA. "Mhe. Heche alifika Polisi Tarime kwa ajili ya kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake, katika hali ya kushangaza naye akawekwa chini ya ulinzi na RCO na baadae kuelezwa kuwa alikuwa akitafutwa kwa makosa mawili  "Kosa la kwanza ni Kauli aliyoitoa mapema mwaka huu katika mkutano wa hadhara Sirari ya kwamba atapeleka hoja bungeni aiombe serikali ihalalishe kilimo cha bangi na pili kauli yake ya hivi karibuni kuhusu kuzuia shughuli za ACACIA Nyamongo kufuatia Kauli ya Rais kwamba mgodi huo haupo kihalali nchini." alisema Marwa Ryoba Aidha Mb...

NEC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA SERIALLY

Image
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani (Kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la kuhifadhia Mashine za BVR. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi.   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama akitazama moja ya Daftari la Wapiga Kura alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani na Kushoto ni Afisa TEHAMA wa Tume Bi. Mwamvita Solo. Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Julius Kobelsiki akitoa ufafanuzi kuhusu Mashine ya kuandikisha Wapiga Kura ya BVR kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Ofi...

Uchaguzi Kenya 2017: Mabalozi wataka wanaowania wakubali uamuzi wa wananchi

Image
Image caption Katika baadhi ya maeneo Kenya, matembezi ya kuhimiza amani wakati wa uchaguzi yameandaliwa Mabalozi wa nchi za Magharibi wametoa wito kwa wagombea katika uchaguzi mkuu nchini Kenya kujiepusha na fujo na kuwahimiza wafuasi wao kutozua ghasia. Mabalozi hao wamesema viongozi wana wajibu wa kukataa ghasia na uchochezi. "Wagombea wanaposhindwa au washinde, wanafaa kuwa tayari kuukubali uamuzi wa wananchi kwa rehema na unyenyekevu," taarifa ya mabalozi hao imesema. Pande zote mbili zinafaa kuheshimu uhuru wa mahakama na ziwe tayari kutatua mizozo kuhusiana na uchaguzi kwa Amani "kupitia mahakama na si kuandamana kwa fujo barabarani." Chama cha Jubilee Jumatano kilikuwa kimemuomba Jaji Mkuu David Maraga amuondoe Jaji George Odunga kutoka kwenye majaji watakaosikiliza kesi kuhusu uchaguzi. Chama hicho kilikuwa kimesema Jaji Odunga ana uhusiano na baadhi ya viongozi wa muungano wa upinzani Nasa na hawezi kutarajiwa atoe uamuzi wa haki bila kuegeme...