Kim Jong-un: Tutarusha makombora zaidi Pacific
Haki miliki ya picha Image caption Baraza la usalama la umoja wa mataifa UN limeishutumu Korea Kaskazini. Vyombo vya habari vya taifa hilo pia vilirejelea vitisho katika kisiwa cha Marekani cha Guam katika bahari ya Pacific ambacho imesema inamiliki kambi ya uvamizi wa kijeshi wa Marekani. Kombora lililorushwa siku ya Jumanne lilipitia juu ya kisiwa cha Japan cha Hokaido na kusababisha hali ya wasiwasi wa kusalama huku raia wakitakiwa kujificha kabla ya kombora hilo kuanguka baharini. Baraza la usalama la umoja wa mataifa UN limeishutumu Korea Kaskazini. Likifanya kikao chake siku ya Jumanne usiku mjini New York , baraza hilo lilitaja urushaji huo wa kombora kama ''ukatili'' na kulitaka taifa hilo kusitisha majaribio yake ya makombora. Lakini matamshi hayo hayakutishia vikwazo vipya dhidi ya Pyongyang. Korea Kaskazini mara kwa mara imekuwa ikifanyia majaribio makonbora yake katika miezi ya hivi karibuni, licha ya kupigwa marufuku kufanya hivyo chini ya s...