Posts

Chama cha mawakili Kenya chamkosoa Uhuru Kenyatta

Image
Haki miliki ya picha FACEBOOKK Image caption Rais wa LSK Isaac Okero Chama cha mawakili nchini Kenya LSK kimemkosoa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya dhidi ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake. Rais wa LSK Isaac Okero katika taarifa siku ya Jumamosi alimkosoa rais Kenyatta kwa kumtaja jaji mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa ''wakora''. Rais Kenyatta alitoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wafuasi wake katika soko la Burma mjini Nairobi siku ya Ijumaa muda mfupi baada ya mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufutilia mbali uchaguzi wake. Bwana Okero alisema: Matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais Uhuru Kenyatta achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya. Amesema kuwa rais Kenyatta anapaswa kulinda haki ya majaji na idara yote ya mahakama. Bwana Okero amesema kuwa ijapokuwa rais...

Jaji jasiri aliyebatilisha uchaguzi wa urais Kenya

Image
Haki miliki ya picha EPA Image caption Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti. Wakenya wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara ya huru wa mahakama. Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day. Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa wanachama wa kanisa hilo. Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya ya siku ya Sabato kuisha. ...

Wanafunzi 7 wafariki katika moto uliochoma bweni Kenya

Image
Image caption Maafisa wa polisi wakishika doria nje ya shule ya Moi Girls liliopo jijini Nairobi nchini Kenya Wanafunzi saba wamefariki na makumi wengine wakijeruhiwa baada ya moto kuchoma bweni la shule ya Moi Girls mjini Nairobi. Waziri wa elimu Fred Matiang'i amesema kuwa wanafunzi wengine 10 walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini. Wawili kati ya 10 wako katika hali mbaya ,kulingana na madaktari huku wengine wanane wakiwa hawako katika hali mbaya. Takriban wanafunzi 10 wamerodheshwa kuwa hawajulikani waliko kulingana na kitengo cha habari cha maafisa wa msalaba mwekundu katika shule hiyo. Image caption Baadhi ya wazazi na wakaazi wa eneo la shule hiyo waliojitokeza kujaribu kuwajulia hali wanawao katika shule hiyo Matiang'i amesema kuwa shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na sababu ya moto huo. Waziri huyo hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa k...

Uhuru Kenyatta: Idara ya mahakama ina 'tatizo

Image
Haki miliki ya picha IKULU KENYA Image caption Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'. Alikuwa akizungumza katika hotuba uliopeperushwa moja kwa moja na runinga siku moja tu baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi wake na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku sitini. Rais Kenyatta alisema kuwa ataiangazia idara ya mahakama ,mbali na kurejelea ujumbe wake kwamba atauheshimu uamuzi wa mahakama hiyo. Wameonya kuikabili idara hiyo baada ya uchaguzi ''Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali. Matokeo ya magavana yalitangazwa na hakuna mtu al...

Ni nini kinachofanyika ubongoni mwa mtu akipiga miayo.

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Kupiga Miayo Unaweza kuwa unapiga miayo hivi sasa wakati ukisoma taarifa hii - ni wa kuambukiza. Sasa watafiti wamekuwa wakichunguza kinachofanyika ubongoni ili kuchochea hali hiyo. Timu ya watafiti katika Chuo kikuu cha Nottingham, imegundua kinachofanyika kwenye sehemu ya mwendo ndani ya ubongo wa binadamu. Sehemu ya primary motor cortex pia inatumika pakubwa kwenye hali kama Tourette's syndrome, yaani kinachofanyika wakati mtu anapopatwa na ugonjwa wa neva. Kupiga miayo mara kwa mara, ni dalili ya echophenomena - yaani namna ya kuiga maneno ya mtu mwingine matendo bila ya kujua. Hali hii ya Echophenomena pia inaonekama katika Tourette's, pia katika hali ya mtu kuugua kifafa na tawahudi. Haki miliki ya picha SUPPLIED Image caption Watafiti hao walitumia kifaa hichio ambacho kinajulikana kitaalamu kama transcranial magnetic stimulation Ili kufanyia uchunguzi kile kinachofanyika ndani ya ubongo wa mtu wakati wa...

Vikwazo vya Marekani vyaathiri utalii wa Korea Kaskazini

Image
Image caption Sekta ya utalii inakua kwa kasi Korea Kaskazini Zuio la Marekani juu ya raia wake kuingia nchini Korea Kaskazini limeongeza madhara,wakati huu ambapo kumeibuka hali ya kusuguana baina ya mataifa hayo mawili. Zuio hilo lilitolewa baada ya mwanafunzi kutoka Marekani Otto Warmbier kufariki punde tu alipoachiliwa kutoka gerezani Korea Kaskazini. Marekani imesema ni muhimu kufanya hivyo kwa lengo la kuwaweka salama wananchi wake. Kwa raia yeyote wa Marekani atakayekiuka sheria hiyo, atakumbana na adhabu ikiwemo kunyanganywa hati ya kusafiria. Marekani imesema itaruhusu tu wananchi wake kusafiri kwenda Korea Kaskazini kwa sababu muhimu ikiwemo uandishi wa habari ama utoaji wa misaada ya kibinaadam. Waandaaji wa ziara za kitalii wanasema kuwa takribani wamarekani 1,000 hutembelea Korea Kaskazini kila mwaka. Wageni wengine ambao huingia Korea Kaskazini kwa wingi kama watalii ni raia wa China. Siku ya Alhamis, waendeshaji wa biashara ya utalii waliwaondoa rai...

Jiwe kubwa sana kupita karibu na dunia

Image
Jiwe kubwa zaidi kuwahi kupita karibu na dunia katika kipindi cha karibu karne moja linatarajiwa kupita karibu na sayari ya dunia umbali wa karibu maili milioni 4.4 , kimesema kituo cha masuala ya anga za juu cha Marekani, Nasa. Vipimo vya Florence vilikadiria umbali wa maili 2.7 sawa na kipenyo cha 4.4 na kwamba jiwe hilo halina tisho kwa dunia kwa karne zijazo Mawe mengine yaliyowahi kupita karibu na dunia, yalikadiriwa kuwa ni madogo sana. Mawe hayo ambayo yana umbo la vifusi upande wa kushoto ni masalia yaliyobaki wakati wakuundwa kwa jua na sayari. Jiwe la Florence - lililogundulika mnamo mwaka 1981- linaweza kuwa mara 18 ya wastani wa umbali baina ya dunia na mwezi. "Florence ni jiwe kubwa zaidi kuwahi kupita karibu na dunia yetu tangu kuanzishwa kwa mpango wa shirika la anga za mbali la Marekani NASA wa kuchunguza na kubaini mawe yaliyopo karibu na dunia ," Amesema Paul Chodas, meneja wa kituo cha NASA kinachochunguza vitu vilivyopo karibu na dunia kat...