Posts

Marekani yatathmini kufunga ubalozi wake Cuba

Image
Image caption Zaidi ya wafanyakazi 20 wa Marekani wameathirika na mashambulizi hayo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Washington inathamini iwapo ifunge ubalozi wake nchini Cuba, baada ya kutokea mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wake. Sasa zaidi ya wafanyakazi 20 wa ubalozi wa Marekani wameripotiwa kuwa na matatizo ya kupoteza uwezo wa kusikia au kupatwa na mfadhaiko kutokana na sauti hiyo. Marekani imeiambia Cuba kuwa ina jukumu la kuwalinda wafanyakazi wote wakigeni wakiwemo . Cuba imekana kuhusika na swala hilo huku uchunguzi zaidi ukiendelea .kujua chanzo cha watu hao kukumbwa na matatizo hayo ya kiafya wanayoyauzungumzia. .

Watu 20 wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakamatwa Zanzibar

Image
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja linawashikilia watu 20, ambao ni wanawake(12) na wanaume(8) kwa tuhuma za kukutwa wakifundishana kufanya mapenzi ya jinsia moja. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib, Hassan Nassir amesema watu hao wamekamatwa wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuzitambua haki zao yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa jina la Bridge Initiative. “Ni kweli tuliweza kuwakamata kwa sababu walikuwa wakishiriki katika mapenzi ya jinsia moja kitu ambacho ni kinyume na sheria kisiwani zanzibar na ni ukiukaji wa sheria za Tanzania”, alisema Hassan pia akaongeza kuwa polisi wataongeza doria zao dhidi ya makundi kama hayo. Mwezi michache iliopita Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed alitangaza vita kwa wanaojihushisha na biashara hiyo haramu na alipiga ‘stop’ taasisi zinazofadhiri watu hao.

Tukio la Kupigwa Risasi Lissu Lilivyofunika Mkutano wa Bunge

Image
Mkutano wa Nane wa Bunge la Kumi na Moja umemalizika huku tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu likifunika mambo mengine manne muhimu yaliyojitokeza. Lissu alijeruhiwa Septemba 7 akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikopatiwa huduma ya dharura kabla ya kuhamishiwa Nairobi, Kenya kwa matibabu zaidi kwa kile ambacho familia na wabunge wenzake wa upinzani walikieleza kuwa ni kuhofia usalama wake. Tukio hilo na mengine yaliyoambatana nalo yameonekana kujadiliwa zaidi kiasi kufunika shughuli nyingine za vikao vya Bunge. Shambulio hilo liliwashtua na kuwaogofya wabunge kiasi cha Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe kuomba mwongozo wa Spika Septemba 8 akisema tukio kama hilo halijawahi kutokea katika historia ya nchi. Bashe alisema linaogofya kwa sababu matukio mengine yaliyolitangulia ya kupotea kwa Ben Saanane ma kutishiwa bastola kwa Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, hawajasikia ta...

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Apiga Marufuku Watumishi wa Umma Kukamatwa Hovyo

Image
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepiga marufuku viongozi wa Serikali kuwakamata na kuwaweka rumande watumishi wa umma bila kufuata sheria na taratibu za utumishi. Gambo alisema juzi kuwa siku za hivi karibuni kumejitokeza matukio ya baadhi ya viongozi kuwaweka rumande watendaji wa Serikali bila kufuata taratibu. “Kama mtendaji alikosea kuna taratibu zake, kuna masuala ya kiutumishi, kuna ya kijinai na ya uchunguzi, hivyo ni busara kufuata taratibu,” alisema. Gambo aliwataka viongozi kutumia vyombo vilivyowekwa na Serikali kutatua matatizo ikiwamo, Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na pia kufuata sheria za utumishi wa umma. Pia, aliwataka watumishi wa umma mkoani Arusha kufanya kazi kwa kushirikiana na kuepuka majungu kwa kuwa wote wanawajibika kwa wananchi. “Fanyeni kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima katika halmashauri zenu na wilaya kwa jumla,” alisema Gambo. Awali, Mkurugenzi wa Halmasha...

Makubwa ya Magazeti ya TZ leo 17.. Dini, Michezo na Hardnews

Image
Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo September 17  2017  kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

Mambo matano ambayo hukufahamu kama yanasababisha Saratani

Image
Magonjwa ya saratani yanatajwa na taasisi na wataalamu mbalimbali wa afya duniani kuwa yanaongezeka kwa kasi kubwa hususani kutokana na jinsi ya maisha ya mtu yaani life style na sababu nyingine nyingi. Vifuatavyo ni vitu vitano ambavyo humweka mtu kwenye hatari kubwa sana ya kupata saratani 1. Ulaji wa vyakula vilivyosindikwa Hivi ni vile vyakula ambavyo vinakuwa vimetolewa kwenye hali ya chakula asili na kuwekewa kemikali mbalimbali kama viungo na vinginevyo ili kubadili ladha, muonekano na sababu nyingine. Kwa mujibu wa wataalamu, chakula asili chochote kikichanganywa na aina zozote za kemikali husababisha maambukizi ambayo huletea shida mwilini hususani kwenye mmng’enyo wa chakula na utumbo. 2.Maambukizi ya vijidudu Maambukizi yoyote ya vijidudu vinavyoweza kupelekea magonjwa mbalimbali pia huweza kukua, kukomaa na kusababisha saratani. Kwa mfano, wataalamu nchini Canada wameeleza kuwa maambukizi ya Kisukari cha aina B na C husababisha ugonjwa wa s...

Aguero afunga 'hat-trick' na kuisadia Man City kuicharaza Watford 6-0

Image
Haki miliki ya picha HUW EVANS PICTURE AGENCY Image caption Sergio Aguero alifunga hat-trick na kuisadia Manchester City kupanda katika kilele cha jedwali la ligi baada ya kuwashona Watford mabao sita bila jibu. Sergio Aguero alifunga hat-trick na kuisadia Manchester City kupanda katika kilele cha jedwali la ligi baada ya kuwashona Watford mabao sita bila jibu. Watford ambao walikuwa hawajafungwa wangepanda hadi katika kilele cha jedwali la ligi iwapo wangepata ushindi dhidi ya kikosi cha Guardiola, lakini walishangazwa na safu ya mashambulizi ya City ambayo imefunga mabao 15 katika mechi tatu. Aguero alianza kwa kufunga mpira wa adhabu uliopigwa na Kevin De Bruyne kabla ya kuugusa mpira karibu na goli na kupata bao la pili baada ya dakika nne na hivyobasi kufanya mambo kuwa 2-0 kufuatia pasi nzuri kutoka kwa David Silva. Gabriel Jesus aliongeza bao la tatu likiwa ni lake la tano msimu huu baada ya kufunga bao zuri kutokana na pasi iliopigwa na Aguerro. Na licha ya...