Mambo matano ambayo hukufahamu kama yanasababisha Saratani


Magonjwa ya saratani yanatajwa na taasisi na wataalamu mbalimbali wa afya duniani kuwa yanaongezeka kwa kasi kubwa hususani kutokana na jinsi ya maisha ya mtu yaani life style na sababu nyingine nyingi. Vifuatavyo ni vitu vitano ambavyo humweka mtu kwenye hatari kubwa sana ya kupata saratani
1. Ulaji wa vyakula vilivyosindikwa
Hivi ni vile vyakula ambavyo vinakuwa vimetolewa kwenye hali ya chakula asili na kuwekewa kemikali mbalimbali kama viungo na vinginevyo ili kubadili ladha, muonekano na sababu nyingine.
Kwa mujibu wa wataalamu, chakula asili chochote kikichanganywa na aina zozote za kemikali husababisha maambukizi ambayo huletea shida mwilini hususani kwenye mmng’enyo wa chakula na utumbo.
Image result for burger
2.Maambukizi ya vijidudu
Maambukizi yoyote ya vijidudu vinavyoweza kupelekea magonjwa mbalimbali pia huweza kukua, kukomaa na kusababisha saratani. Kwa mfano, wataalamu nchini Canada wameeleza kuwa maambukizi ya Kisukari cha aina B na C husababisha ugonjwa wa saratani ya ini.
Image result for infection
3. Uvutaji wa sigara
Hili ni tatizo kubwa sana linalopelekea magonjwa ya saratani duniani hususani saratani ya mapafu. Uvutaji sigara pia huathiri zaidi wale ambao hawavuti sigara lakini huvuta moshi huo wa sigara pindi wanapokua karibu na wanao vuta sigara. Inaelezwa kuwa vifo vya watu 600,000 duniani huwa ni vya wanaovuta moshi wa sigara za wafugaji.
Pia inaelezwa kuwa uvutaji wa sigara husababisha magonjwa ya moyo, kiharusi, saratani, na magonjwa mengine sugu ya mfumo wa upumuaji. Uvutaji sigara kawaida huendana na unywaji wa pombe na hivyo inaelezwa kuwa athari zake zinakaribiana.
Image result for smoking
4. Mlo mbaya (Poor diet)
Hii pia inaweza kuelezewa kama ulaji usio wa afya. Na hii ni kwa jinsi ya kula vitu ambavyo huleta matatizo katika mwili. Moja ya vitu vinavyotajwa kuwa sehemu ya mlo mbaya ni pamoja na kutokula mboga za majani nyingi na matunda, kuzidisha ulaji wa nyama nyekundu na iliyosindikwa, kula mafuta mengi, ulaji wa chumvi nyingi na mengineyo.
Inaelezwa pia kuwa nyama aina ya ‘berbacue’ husababisha saratani za matiti na kongosho.
Image result for poor diet
5. Uzito wa kupitiliza
Hii kutokana na kutokua na tabia ya kufanya mazoezi ya mwili. Uzito mkubwa mara nyingi huchangiwa na aina za vyakula watu wanavyokula. Tatizo hili huweza kuondoka kabisa endapo muhusika ataamua kufanya mazoezi ya mwili. Kufanya mazoezi kunafaida za kupunguza fetma yaani ‘obesity’, kuimarisha nishati na kinga ya mwili, hali ya moyo na mapafu pia.
Image result for overweight

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi