Posts

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne.

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Henrikh Mkhitaryan Arsenal wako makini kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan 28, kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamleta mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29, huko Old Trafford. (Guardian) Manchester City wamejitoa katika makubaliano ya kumsaini Sanchez na pesa zilizoitishwa na ajenti wake. (Goal) Refa amrushia teke mchezaji kisha kumpa kadi Ufaransa Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux Malcom siku ya Jumapili na wanatarajia kulipa pauni milioni 40 kwa mBrazil huyo wa miaka 20. (Guardian) Arsenal na Chelsea wanammezea mate mshambuliaji wa Watford raia wa Brazil Richarlison 20. (Sun) Haki miliki ya picha PA Image caption Andy Carroll Chelsea bado wako makini kumsaini mshambuliaji wa mwezi Januari kwa mkopo huku Andy Carroll wa West Ham akiwa katika nafasi nzuri wa kusainiwa. (Telegraph) Manchester United wako tayari kumpa kipa wa miaka 27 David de Gea mkataba mpya amboa ...

Watu 20 wameuawa katika mapigano Libya

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Mashambulizi yanayofanywa Libya Watu 20 wameuawa kufuatia mapigano yaliyotokea kati ya makundi ya wanamgambo hasimu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Mapigano hayo yamesababisha kusitishwa kwa safari za ndege, katika uwanja wa kijeshi wa Maitiga, ambao ndio wa pekee wa kimataifa mjini Tripoli. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters ndege zipatazo tano zimeathiriwa na mapigano hayo. Seikali ya Maridhiano ya kitaifa ya Libya imesema shambulio hilo ni jaribio la kundi moja la wapiganaji kuachiliwa kwa wafuasi wake waliokuwa wakishikiliwa na kundi wanalopingana nalo. Ghasia za mara kwa mara zimekuwa zikitokea mjini Tripoli tangu mweaka 2011.

Watoto waliofungwa minyororo wapatikana kwenye nyumba California

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto. Wazazi wawili wamekamatwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa mateka nyumbani kwao wakiwemo wengine waliofungiwa kwa vitanda vyao kwa minyororo na vifuli. David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto. Watu hao 13 walio na umri wa kati ya miaka miwili na 29, walipatikana kwenye nyumna huku Peris kilomita 95 kusini mashariki mwa Los Angeles. Wote hao wanaaminiwa kuwa ndugu. Maafisa waligungua hilo siku ya Jumapili wakati mmoja wa watu hao alifanikiwa kuponyokana na kupiga namba ya dharura akitumia simu ambayo alipata ndani ya nyumba. Msichana huyo ambaye polisi wanasema alionekana kuwa na umri wa miaka 10, alidai kuwa ndegu zake wengine 12 walikuwa wakishikiliwa na wazazi wao. Polisi baadaye walipat...

MAGAZETI YA TZ NA NJE LEO DECEMBER 21,2017

Image

Swansea City yamtimu kocha Paul Clement

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Klabu ya Swansea City, imemfuta kazi meneja wake Paul Clement Klabu ya Swansea City, imemfuta kazi meneja wake Paul Clement kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo msimu huu. Clement mwenye miaka 45 alichukua jukumu la kuiongoza Swansea, mwezi Januari mwaka huu na kuisaidia kutoshuka daraja na kumaliza katika nafasi ya 15 msimu uliopita. Katika msimu huu mpaka sasa Swansea wamecheza michezo 18, na wameshinda michezo mitatu ya ligi wakiwa wanaburuza mkia kwa alama 12. Mwenyekiti wa Swansea Huw Jenkins, ametoa taaarifa kwa kusema klabu imelazimika kufanya hivyo ili kuweza kuisaidia timu kufanya vizuri.

Bristol City yaitupa nje ya michuano Man United

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Klabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao Klabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao kwa kuwaondosha mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Manchester United.  Bristol walianza kuzifumania nyavu za United kwa goli la Joe Bryan, katika dakika ya 51 ya mchezo iliwchukua dakika saba tu kwa Manchester United, kusawazisha goli hilo kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic. Shujaa wa Bristol City alikuwa ni kiungo Korey Smith aliyefunga goli la ushindi katika dakika za lala salama. Nayo Chelsea wakatinga katika hatua ya nusu fainali kwa kuwatungua AFC Bournemouth kwa magoli 2-1 . Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mfungaji wa bao la Chelsea Kiungo Willian Borges da Silva, ndie aliyeanza kupatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 13 ya mchezo Bournemouth wakasawazisha goli hilo katika dakika ya tisini kupitia kwa kiungo Daniel Gosling, Mshambulia...

Mwimbaji wa Korea Kusini Kim Jong-hyun kuzikwa leo

Image
Image caption Kim Jong-hyun alikua mwanamuziki mashuhuri Korea Kusini Mazishi ya mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun, yanafanyika leo hii mjini Seoul. Mwanamuziki huyo ambaye pia alikua mtangazaji wa radio, mwandishi wa vitabu na mtunzi wa nyimbo, alikutwa amekufa katika tukio linalotajwa kuwa la kujiua. Umati mkubwa wa watu umekusanyika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho, huku mwili wake ukibebwa na gari aina ya limousine nyeusi kutoka hospitalini alipohifadhiwa kwa takriban siku tatu. Image caption Picha yake iliwekwa hospital mjini Seoul Ibada ya kumuaga kifamilia ilifanyika mapema pia mjini Seoul. Mwanamuziki huyo aliyekua na miaka 27 akiimbia bendi ya Shinee,alikutwa ameanguka kutoka ghorofa moja refu la kupangisha siku ya Jumatatu.