Mwimbaji wa Korea Kusini Kim Jong-hyun kuzikwa leo
Mazishi ya mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun, yanafanyika leo hii mjini Seoul.
Mwanamuziki huyo ambaye pia alikua mtangazaji wa radio, mwandishi wa vitabu na mtunzi wa nyimbo, alikutwa amekufa katika tukio linalotajwa kuwa la kujiua.
Umati mkubwa wa watu umekusanyika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho, huku mwili wake ukibebwa na gari aina ya limousine nyeusi kutoka hospitalini alipohifadhiwa kwa takriban siku tatu.
Ibada ya kumuaga kifamilia ilifanyika mapema pia mjini Seoul.
Mwanamuziki huyo aliyekua na miaka 27 akiimbia bendi ya Shinee,alikutwa ameanguka kutoka ghorofa moja refu la kupangisha siku ya Jumatatu.
Comments
Post a Comment