Bristol City yaitupa nje ya michuano Man United

city


Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKlabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao

Klabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao kwa kuwaondosha mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Manchester United. 
Bristol walianza kuzifumania nyavu za United kwa goli la Joe Bryan, katika dakika ya 51 ya mchezo iliwchukua dakika saba tu kwa Manchester United, kusawazisha goli hilo kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic.
Shujaa wa Bristol City alikuwa ni kiungo Korey Smith aliyefunga goli la ushindi katika dakika za lala salama.
Nayo Chelsea wakatinga katika hatua ya nusu fainali kwa kuwatungua AFC Bournemouth kwa magoli 2-1 .

chelseaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMfungaji wa bao la Chelsea

Kiungo Willian Borges da Silva, ndie aliyeanza kupatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 13 ya mchezo
Bournemouth wakasawazisha goli hilo katika dakika ya tisini kupitia kwa kiungo Daniel Gosling, Mshambuliaji hatari wa Chelsea Alvaro Morata akawapeleka Chelsea nusu fainali kwa goli la dakika ya 91.
Michezo ya nusu fainali itapigwa januari 9, mwakani kwa Chelsea kucheza na Arsenal na Bristol City kucheza na Manchester City.

Comments

Popular posts from this blog

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA