Chidi benzi asimulia story nzima
jinsi ilivyokuwa hadi kukamatwa na dawa za kulevya Airport.
Rashid Makwiro a.k.a Chidi Benz ambaye ameachiliwa kwa
dhamana Jumatano wiki hii, amesimulia jinsi ilivyokuwa hadi kukamatwa Ijumaa
iliyopita Oct.24 na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Julius
Nyerere.
Chidi alizungumza na Soudy Brown kupitia So So Fresh
ya Clouds FM jana.
“Sikuwaambia natumia, niliwaambia dawa ambazo nilikuwa
niko nazo lazima nitakuwa nimeconfuse kipindi ambacho natumia nilikuwa ofcoz
naweka weka naficha ficha kwenye nguo nguo zangu na nini, so nimewambia maybe
kwasababu hiyo nguo sijawahi vaa ndio mara ya kwanza…huwa naweka mashati kadhaa
nayatundika tu hivi yako kama kumi kumi na tano, huwa nikivaa najua hili
nasafiri nalo au nazunguka tu leo round za town baadae nikilivua nalitupa tu si
unajua sisi mara nyingi nguo ukivaa unakuwa unavaa mara moja labda hivyo. So
nahisi lazima ile dawa nilikuwa nimeiweka labda niliiweka au nimeficha coz
nilikuwa naweza nikachukua hivi enzi zile sitaki mtu aone na nini naiweka
kwenye mfuko naiacha hapo na hilo shati sijawahi vaa ndo nimelivaa juzi. “ alisema Chidi Benz.
“Shetta alinipigia simu akaniambia tunaondoka leo
nikamwambia ooh yeah? Ooh yeah leo fasta, na mimi sasa hivi nakaa Tegeta unajua,
so nikachukua lile shati fasta sio la kupiga pasi ni kama hili nililovaa hapa
nikalichukua tu nikalipiga na jeans hivyo. Nikaenda zangu airport, niko airport
nikamwambia Shetta namtania tu hivyo namwambia mdogo wangu nimebeba mambo
nimebeba mambo [kicheko], nimebeba mambo kibao yale mabegi yamejaa yote haya
yote mabegi sina nguo wala viatu wala nini hapa nina mambo tu like namtania
unajua, lakini sasa nafika pale nasachiwa ndo nakutana na hiyo dawa”.
Aliendelea,
“Imagine nimekutwa na dawa kwenye mfuko wa shati
kushoto unajua si kama nimeficha au nimefanya nini. Of course kila mtu anaongea
cha kwake hamna yule muongo atakuwa hivi hamna mteja yule of course, so saivi
lazima nikubali kwa kila mtu anachokiongea as long kwamba watu walikuwa
hawasaidii chochote time ambayo sijakamatwa au sijakutwa hamna kitu chochote
walikuwa mtu nasaidiwa au naambiwa kwahiyo naona kawaida tu.
Lakini si kitu nimepanga si kitu nilikuwa nimeplan
unajua nimekutwa nayo mimi mwenyewe ndio nimejisachi, si yeye sijakamatwa mimi
mwenyewe nimejisachi nimezitoa kushoto kulikuwa na pesa kulia pesa kushoto pesa
tena akaniambia we pesa pesa akaniambia hapa mfukoni juu kuna nini, nikamwambia
hii I think ni uchafu uchafu tu natoa hivi nakuta vidude kama kadhaa hivi
naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia bwana hii nini nikamwambia
hii…dawa but sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinaadam nilikuwa kama kidogo
akili imeniruka kuja kugundua kwamba ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe unajua…
Yaani kwanza nakwambia kwasababu hata yeye wakati
natoa hizo pesa nilikuwa kama namtania yule jamaa ananiambia mfuko wa nyuma
namwambia hizi pesa huku pesa, hii karatasi yangu ya mashairi nataka niandike,
hii huku pesa akaniambia na hapa juu nikamwambia hapo juu hamna kitu ni uchafu
uchafu tu, hee natoa hivi nakutana na kimkanda unajua so like kama nilipigwa na
butwaa hivi unajua.”
Chidi
alisema alijaribu kuwaomba wana usalama wamuelewe na kumsamehe lakini
ilishindikana.
“Nikajaribu kuwaomba jamaa nikawaambia bwana sorry
kuna time nilikuwa natumia hizi vitu but nikaachana nazo, so wakati naachana
nazo ofcoz zamani nilikuwa sio mtu wa kununua kimoja kimoja nilikuwa nanunua
labda kadhaa unajua so navyohisi labda siku nilizichomeka kwenye kamfuko haka
ka juu wa shati nikaziweka hapa nimesahau nguo nimeivaa tu ghafla nimesahau
kiukweli, so please kama mnaweza kunielewa mkanisamehe please, hakuna
ninachosafirisha hakuna nini mabegi yangu haya hapa mnaweza mkanisachi
nisachini kote, wakasachi kila begi kila kitu hakuna kitu sina kitu kingine,
nilikuwa na spika nilikuwa na viatu nilikuwa na nguo done.” alimaliza Chidi Benz
Kesi yake imepangwa kusikilizwa tena November 11.
Comments
Post a Comment