TAARIFA YA TUKIO LILILOTOKEA UBUNGO
PLAZA KATIKA MKUTANO WA MWALIMU NYERERE FOUNDATION
Mkutano ulifanyika kuanzia
saa 1520hrs ukiwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu mh. Joseph Sinde Warioba.
Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za
kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na ITV na maudhui yake kimtazamo
ulilenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya tume ya Warioba na
ile ya Mh. Sitta na tume yake. Baada ya Mh. Warioba kuelezea kwamba Muungano
sio tunu ila
ni urithi ndipo wakereketwa wa
upande wa Mh. Sitta walipoinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba
iweje wajadili mapendekezo ya katiba ya Mh. Sitta ambayo wao wameshaikubali?
Baada ya mabango yale kuinuliwa yakazua tafrani ambapo walishauriwa kutoyainua
kwa sababu haukuwa mkutano wa kisiasa na wakanyang’anywa na kuyachana ndipo
vurugu/kashfa/matusi yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha
kushikana, kusukumana na kurushiana viti. Katika tafrani hiyo mh. Warioba
alipigwa kibao na Mh. Paulo Makonda- ambaye ni katibu wa UVCCM TAIFA. Mtuhumiwa
huyu pamoja na wengine wanne wamekamatwa kwa mahojiano. Upelelezi unaendelea na
juhudi za kuwapata wengine zinaendelea.
Comments
Post a Comment