mwanamke aishi na wanaume wawili kiunyumba miaka nane bila kutambuana.
MWANAMKE AISHI
KINYUMBA NA WANAUME WAWILI KWA MIAKA NANE BILA KUTAMBUANA MBEYA
Juliana Josia(22)kushoto anaedaiwa kuishi na wanaume
wanaume wawili kwa zaidi ya miaka 8 bila kutambuana akiwa na Mume wake halisi
Rogers ofisini kwa mtendaji
Juliana Josia(22)kushoto akiwa na barozi Dinde
Bwana Rogers akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa
kwenda kituo cha polisi
Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juliana
Josia(22)amezua utata hivi karibuni baada ya kugunduliwa akishi na wanaume
wawili kwa muda wa miaka minane bila wanaume hao wawili kujitambua.
Hayo yalibainika katika kituo cha Polisi Kati Jijini Mbeya
baada ya Mwanamke huyo kudai kuporwa mtoto mgogoni jinsi ya kike mwenye umri wa
miaka miwili eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya kutishiwa na Biton Bomani
Mwashilindi mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.
Juliana alidai kuporwa mtoto na Biton Oktoba 27 mwaka huu
majira ya saa nne asubuhi alipokuwa akielekea soko la Sido kwenye shughuli zake
za biashara na kutoa taarifa kituo cha Polisi Mwanjelwa na baadaye kituo kikuu
kati na kufunguliwa jalada la wizi wa mtoto namba MB/RB/9384/2014 ambapo juhudi
za kumtafuta zilifanikiwa baada ya taarifa kutolewa Kituo cha Radio cha Bomba
FM Mbeya ndipo alipojisalimisha mwenyewe akiwa na mtoto Zalida Rogers(2).
Hata hivyo katika hali ya mshangao Biton alifika katika
kituo cha Polisi Kati akiwa na Cheti cha kuzaliwa na kadi ya kliniki ambapo
kinaonesha mtoto Zalida kuzaliwa kituo cha Afya Ruanda Mwanjelwa na kuonesha
kuzaliwa 18/08/2012 wazazi wakiwa ni Juliana Josia na Biton Mwashilindi.
Biton alidai mbele ya Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi
kuwa Juliana ni mpenzi wake kwa muda wa miaka nane na kwamba walikuwa
wakikutana katika nyumba ya kulala wageni kila alipomhitaji na walikuwa
wakipanga katika nyumba hiyo kwa siku saba kila wanapokutana hali ilyofanya
watu wanaosikiliza tukio hilo kituo cha Polisi kushikwa na butwaa akiwemo mume
halali Rogers Halinga na mke wa Biton ambaye alimtunza mtoto kwa siku nne.
Akijieleza kwa kujiamini Biton alidai kuwa hata mtaji wa
biashara alimpatia yeye na hata wazazi wake Biton walioko Itaka Mbozi
walimtambua mtoto Zalida na kwamba jina la mtoto alipewa na ndugu zake na hata
aliowahi kuugua alikwenda Itaka Mbozi na kukaa kwa wazazi wa Biton kwa zaidi ya
juma moja.
Kwa upande wa Rogers yeye alisema mtoto Zalida ni wa kwake
na kwamba aliondoka kwao akiwana na ujauzito wa miezi mitano na kwamba yeye
alijua kukorofishana kwao kulitokana na hali ya ujauzito na alikaa kwamba mkewe Juliana alikaa kwao kwa miezi
sita na alipojifungua alirejea kwake na aliohitaji kupata maendeleo ya mtoto
mkewe alidai kuwa kadi ya kliniki imepotea.
Kikao hicho kilichokuwa na mvutano mkubwa kiliahirishwa na
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya kwa kumshikilia Biton kwa kosa la kutorosha
mtoto na kesi ya ugoni na kuwa atafikishwa mahakamani pindi upelelezi
utakapokamilika huku Rogers akikabidhiwa mkewe na mtoto kwa minjili ya kwenda
kuyajenga huko nyumbani kwao Kijiji cha Ishungu Kata ya Ruiwa wilaya ya
Mbarali.
Baba mzazi wa Rogers Mzee Jason Halinga alisema alishangazwa
na kitendo kilichofanwya na mwanamke huyo ambapo alidai kuwa mwanae alioa
kihalali na kufuata mila zote na kulipa mahari lakini alishangazwa na kitendo
cha wazazi wa Juliana kushindwa kuonesha ushirikiano hali inayoashiria kujua
kile kilichokuwa kinafanywa na mtoto wao.
Biton alifika kituo cha Polisi akiwa na mkewe wa ndoa ambapo
naye hakufahamu kuwa mumewe anaishi na mke mwingine nje ya ndoa na kwamba mtoto
Zalida alipoletwa kwake hakuambiwa chochote kile na kwamba ameishi kwenye
mateso ya ndoa kwa muda wa miaka nane huku akifanyiwa vitendo vya kikatili na
mumewe ikwa pamoja na kuambulia kipigo mara kwa mara.
Baadhi ya ndugu wa Rogers walioneshwa kukerwa na baadhi ya
Askari wa ngazi juu katika Dawati la
Jinsia Kituoni hapo ambao walonesha kutojali suala hili huku wakitioa maneno ya
kejeli hali inayotia dosari utendaji kazi wa Dawati hilo na kwamba lipo
kibiashara zaidi na si huduma kama
ilivyo sera ya Jeshi la Polisi.
Hata hivyo hawakusita kuwapongeza Askari wa Kiume walionesha
juhudi hata kufanikwa kupatikana kwa mtoto Zalida na Biton pamoja na rafiki
yake.
Katika sakata hili kama si juhudi za Kamanda wa Polisi
Mkoani Mbeya Ahmed Msangi kuingila kati basi mtoto Zalida asingeweza kupatikana
kama baadhi ya watoto waliotoweka maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya ambao
hawajapatikana mpaka sasa ambapo wananchi wamelalamikia Kituo Kikuu cha Kati kwa
kutochukua hatua za haraka za kukomesha vitendo vya ukatili wa Kijinsia na
baadhi kuamua kumalizana wenyewe mitaani vikiwemo vitendo vya ubakaji ambavyo
vimeshamiri mkoani Mbeya.
Hatima ya ndoa ya Rogers na Juliana itajulikana baada ya
mazungumzo yatayofanyika kwa Mzee Jason Halinga nyumbani kwake Ishungu Kata ya
Ruiwa hivi karibuni kikao kitakutaniha pande mbili za wazai ili kufikia muafaka
katika sakata la aina yake na kwamba hata kubainika kwa sula hili ni kutokana
na Juliana kufumwa na mwanaume mwingine katika chumba ambacho Biton alikuwa awe
na Juliana ndipo alipoamua kulipiza kisasi kwa kutorosha mtoto.
Comments
Post a Comment