Posts

Showing posts from July, 2015

MALAIKA AANGUKA UINGELEZA.

Image
Tukio Lisilo la Kawaida MALAIKA Aanguka Nchini UINGEREZA..Watu Wamiminika Kushuhudia Picha ya karibu ikionesha sura ya malaika huyo na mbawa zake. Tukio lisilo la kawaida limetoa huko Uingereza.... MALAIKA aanguka nchini UINGEREZA na kuifadhiwa sehemu maalum ambapo watu wameanza kumiminika kwenda kumshuhudia Baadhi ya laia waliofika kushuhudia tukio hilo wakiwa hawaamini kilichotokea. Akiwa kahifadhiwa kwenye sehemu maalum,picha ikionesha kwa mbali .

Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo

Image
Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo Sos Mpekuzi blog Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema watu  zaidi  ya 10  wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.   Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma.Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu.

Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa

Image
Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa Ziara ya Obama nchini kenya Shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi. Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa imetua. Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.   ...

Gereza la Guantanamo lakaribia kufungwa

Image
Gereza la Guantanamo lakaribia kufungwa gereza la Guantanamo linamilikiwa na Marekani Ikulu ya White house imesema kuwa mipango ya kulifunga gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba imefikia awamu za mwisho. Rais Barack Obama anasemekana kupatia kipa umbele suala la gereza hilo tangu aingie madarakani mwaka wa 2009 lakini limekumbwa na vizuizi kadhaa.   gereza lililo n aulinzi mkali la Guantanamo Gereza hilo la Guantanamo, ambalo limepewa jina la umaarufu kuwa Gitmo - limekuwa likitumiwa na Marekani kuwazuilia wapiganaji kutoka vita vya Iraq na vya Afghanistan bila kufunguliwa mashtaka yoyote. Rais Obama alitoa agizo la kirais kufungwa kwa kituo hicho mara moja katika siku yake ya kwanza. Lakini baraza la Congress lilikataa kuwahamisha wafungwa wa huko kuwaleta...
Image
Said Alf awakimbia CHADEMA, Ataka ubunge kwa CCM   sos.Mpekuzi blog MBUNGE wa Jimbo la Mpanda Mjini, Bw. Said Amour Alfi (CHADEMA) ni miongoni  mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wamechukua na kurejesha fomu za kuomba kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Nsimbo, Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa CCM mkoani Katavi, Averin Mushi amethibitisha Bw. Arfi kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo hilo.  Alisema makada 23 wamejitokeza kuwania ubunge katika majimbo yote ya uchaguzi mkoani humo ambapo katika Jimbo la Nsimbo, makada ambao wamerejesha fomu ni Bw. Arfi, Shabir Hasanali 'Dallah', Richard Mbogo, Manamba David na Mapesa Frank. Katika Jimbo la Katavi ni Isaack Kamwelwe, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo, Shafi Mpenda, Maganga Kampala na Osca Albano. Kwa upande wa Jimbo jipya la Kavuu, yupo Zumb...

Wabunge wa Chadema Wamkaribisha Edward Lowassa

Image
Wabunge wa Chadema Wamkaribisha Edward Lowassa Baadhi ya wabunge wa Chadema wamezungumzia taarifa zinazosambaa zikieleza kuwapo mkakati wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho, wengi wao wakimkaribisha. Wakati wabunge hao wakikubali kumpokea, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa amesema wananchi wasubiri mambo yatakapokuwa tayari badala ya kutegemea mitandao ya kijamii. “Nitazungumza pale mambo yatakapokuwa sawa, siwezi kuzungumza sasa, subirini… sasa hivi mambo mengi yanazungumzwa kwenye mitandao,” alisema Dk Slaa ambaye pia anatajwa kuwa mgombea wa chama hicho ndani ya Ukawa. Msemaji wa Lowassa, Aboubakary Liongo alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango huo alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa ni suala la mtu binafsi. Hata hivyo, jitihada za kumpata Lowassa jana hazikufanikiwa kwani simu yake iliita pasi na kupokewa. Hivi karibuni, idadi kubwa ya madiwani wa CCM walirudisha kadi zao na kujiunga na Chadema wakisem...
Image
CHADEMA Kumtangaza Mgombea Wake wa Urais LEO Jijini Mwanza Dr.Slaa Baada ya vuta vikuvute ya muda mrefu, hatimaye leo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais katika mkutano maalumu utakaofanyika jijini Mwanza. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi na makao makuu zilisema kuwa leo mgombea huyo atatangazwa mkoani hapa huku zikibainisha kuwa anayepewa nafasi kubwa ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa. Taarifa hizo zimekuja wakati kukiwa na tetesi kuwa chama hicho kilikuwa kinafanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyekuwa anawania urais kupitia CCM na kutemwa katika hatua za awali, huku vyanzo mbalimbali vikisema mazungumzo hayo yanachukua muda mrefu na kuna uwezekano mkubwa wa kutozaa matunda. Jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na baadhi ya wabunge walikaririwa wakitoa matamko ya kumkaribisha ...

Nchimbi Afunguka baada ya CCM Kulikata Jina lake Kwenye Kinyang'anyiro cha Ubunge

Image
Nchimbi Afunguka baada ya CCM Kulikata Jina lake Kwenye Kinyang'anyiro cha Ubunge Aliyekuwa wazili wa mambo ya ndani na mbunge wa songea mjini Emmanuel Nchimbi akitoa hoja bungeni. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi (pichani), amefunguka kuhusu mambo kadhaa na kueleza kuwa  Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa kutofautiana katika vyama vya siasa ni jambo la kawaida katika nchi yenye demokrasia. Dk. Nchimbi alisema hayo jana ikiwa ni siku moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Songea Mjini kuikataa fomu ya kuomba kuwania ubunge aliyochukuliwa na wananchi kwa madai haikuwa imekidhi vigezo. “Ninachowambia Watanzania tuzoee kutofautiana, kutofautiana katika vyama vyetu ni jambo la kawaida katika demokrasia, tunaweza kutofautiana katika mapendekezo, lakini tukifika kwenye maamuzi tunakuwa kitu kimoja kuunga maamuzi tuliyoafikiana na huo ndio utaratibu mzuri wa kujenga demokrasi...

Majambazi 27 wenye silaha wakamatwa mkoani Pwani

Image
Majambazi 27 wenye silaha wakamatwa mkoani Pwani Jeshi la polisi Mkoa wa Pwani  limefanya msako mkali katika mapori mbali mbali  na  kufanikiwa kuwakamata   watuhumiwa  wa ujambazi  27 pamoja na   risasi 153,bunduki 2  mabomu 3  ambavyo  walikuwa wakivitumia katika matukio ya uharifu.   Kwa mujibu wa  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu amesema kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kufanyika operesheni katika magenge yaliyopo vichakani na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wamejificha pamoja na silaha walizokuwa wanazitumia kufanyia uhalifu   Ameongeza kuwa  wameamua kufanya  operesheni  hiyo  kutokana na kuongezeka kwa uharifu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na kuwakamata watuhumiwa hao  ambao wengine walikutwa na vifaa mbali mbali ikiwemo visu mapanga,pamoja na nyaya tatu za milipuko ya mabomu.   Kat...