Al-Shabab washambulia mji wa El Wak karibu na mpaka wa Kenya

Wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia

Kundi la wapiganaji wa Somalia, al Shabaab, limeshambulia mji wa El Wak, karibu na mpaka wa Kenya.
Wapiganaji hao waliingia mjini humo, bila kupata pingamizi yoyote, na kuharibu makao makuu ya serikali ya eneo hilo pamoja na kituo cha polisi.
Hapo awali, wanajeshi wa serikali ya Somalia, walikimbilia Kenya.
Wakuu wa El Wak wanasema al-Shabaab waliwaonya mapema, wakaazi wa El Wak, wasishirikiane na jeshi la Somalia na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Afrika, (AMISOM).
Waliiba msaada wa vyakula, na kuondoka El Wak baada ya saa chache.

Comments

Popular posts from this blog

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA