FIFA yataka mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal urudiwe
Shirikisho la kandanda la Kimataifa FIFA, limeamuru mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal uliofanyika Novemba 12 urudiwe .
Uamuzi huo umetolewa baada ya mwamuzi wa mchezo huo Joseph Lamptey kuvurunda kimaamuzi katika mchezo huo, hivyo ameadhibiwa na Kamati ya nidhamu ya FIFA .
Mchezo huo utarudiwa Novemba 2017 katika kalenda ya kimataifa, kwenye tarehe ambayo itatajwa.
Bafana Bafana waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba wa Teranga katika mchezo huo.
Comments
Post a Comment