Kimbunga Irma chaendelea na uharibifu mkubwa huko Caribbean
Kimbunga Irma kimeelekea visiwa vya Turks na Caicos baada ya kusababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean na kuwaua takriban watu 14.
Visiwa vilivyo nyanda za chini vinaripotiwa kuwa kwenye hatari kubwa kukiwa na uwezekano wa kupigwa na mawimbi ya hadi urefu wa mita 6 kuliko viwango vya kawaida.
Kumeripotiwa uharibifu na mafuriko nchini Haiti ambapo miundo mbinu bado ni mibaya tangu litokee tetemeo la ardhi mwaka 2010.
Irma ni kimbunga cha kiwango cha tano.
Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi cha kimbunga na upepo wake una kasi ya kilomita 280 kwa saa.
Takiban watu milioni 1.2 wameathiriwa na kimbunga Irma na idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa haraka hadi watu milioni 26.
Kuna wasi wasi kuwa ugonjwa unaweza kusambaa kwa haraka maeneo ambapo maji ya kunywa na huduma za usafi zimeathirika, na maafisa wameonya kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.
Irma sasa kiko karibu na visiwa vya Turks na Caicos na huenda pia kikaelekea huko Bahamas.
Kimbunga hicho kinatarajiwa kufika Cuba baadaye kabla ya kupinga jimbo la Florida huko Marekani mwishoni mwa wiki huku mkuu wa shirika la huduma za dharura la Mareknia akitabiri uharibifu mkubwa.
Maandalizi ya kuwasili kimbunga Irma yalifanywa katika visiwa vya Turks na Caicos ambayo ni himaya ya Uingereza yenye vyenye watu 35,000.
Irma pia kilisababisha uharibifu kwa paa za nyumba na kawi katik sehemu za kaskazini mwa Jamhuri ya Dominica.
Nchini Cuba maelfu ya watalii kutoka maeneo ya kistarehe ya pwani wamehamishwa.
Comments
Post a Comment