Juhudi za uokoaji zinaendelea Mexico
Juhudi za kuwatafuta waliofukiwa na kifusi kufuatia Tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Mexico zinaendelea licha ya matumaini madogo, kuwakuta hai.
Wafanyakazi wa majanga ya dharura na wale wa kujitolewa wamekuwa wakichimbua vifusi kwa kutumia mikono. Watu 225 wamefariki nchi nzima kutokana na tetemeko hilo, wakiwemo watoto 21, ambao walikufa wakiwa shuleni Mexico city.
Kuna hofu ya watoto zaidi kufariki kutokana na kwamba walikuwa darasani jengo lilipo poromoka.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kila dakika inahesabika katika kuokoa maisha ya watu.
Watu 52 tayari wameokolewa kutoka katika kufusi katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Tetemeko hilo la ardhi ni la pili kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha mwezi mmoja.
Comments
Post a Comment