Kisiwa cha tajiri Richard Branson chaharibiwa na kimbunga Irma

Richard Branson


Haki miliki ya pichaRICHARD BRANSON
Image captionSir Richard akitathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga Irma

Sir Richard Branson amesema mengi ya majengo na mimea na miti katika kisiwa chake cha Necker katika eneo la Caribbean vimeharibiwa kabisa na Kimbunga Irma.
Necker ni moja ya visiwa 50 ambavyo hujumuisha Visiwa vya Virgin vya Uingereza (BVI).
Sir Richard amesema alitembelea kisiwa kinachokaribia zaidi kisiwa chake cha Necker na kujionea "moja kwa moja ukali na ukatili wa kimbunga hicho".
Kimbunga hicho kiliua watu watano katika eneo hilo la Uingereza.
Waziri mkuu wa BVI ameomba usaidizi wa muda mrefu kutoka kwa Uingereza.
Sir Richard na wenzake wako salama.

NeckerHaki miliki ya pichaRICHARD BRANSON
Image captionMajumba katika kisiwa cha Necker yaliyumbishwa na mengine kuporomoka

Kimbunag Irma kilipitia Visiwa vya Virgin vya Uingereza katikati mwa wiki iliyopita.
Sir Richard amesema: "Tulihisi nguvu kali zaidi za kimbunga chenye nguvu zaidi kuwahi kupiga kutoka Bahari ya Atlantiki. Lakini tulikuwa na bahati sana kwamba tulikuwa na handaki imara ambalo tulikuwa tumelijenga katika Jumba Kuu la Necker na tulikuwa na bahati sana kwamba watu wote waliokuwa kisiwani wakati wa kimbunga wako salama."

Necker IslandHaki miliki ya pichaRICHARD BRANSON
Image captionSir Richard anasema mimea, miti na nyasi katika kisiwa hicho vimeharibiwa

Amesema kinachofaa kuangaziwa zaidi ni "visa vya maelfu ya watu ambao wamepoteza nyumba zao na bishara zao".
Mawasiliano bado yamekatizwa katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Sir Richard kwa sasa yuko katika kisiwa cha Puerto Rico, kilomita kadha magharibi mwa visiwa hivyo vyake.

Necker Island damageHaki miliki ya pichaRICHARD BRANSON

Alisema alikuwa ameenda huko "kuratibu zaidi juhudi za kutumwa kwa misaada zaidi na kusimamia mipango ya ukarabati wa mijengo katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza na maeneo ya Caribbean kwa jumla."
Sir Richard amesema atazungumza na serikali mbalimbali na mashirika ya misaada, pamoja na vyombo vya habari.
Amesema baadaye atarejea pigania zaidi kufanywa kwa Visiwa vya Virgin vya Uingereza kusaidia juhudi za ukarabati.
Visiwa vya Virgin vya Uingereza ni eneo linalojitawala la Uingereza ambalo humtambua Malkia Elizabeth wa Uingereza kama kiongozi wa taifa.
Waziri mkuu wa visiwa hivyo Orlando Smith amesema watahitaji misaada kwa kipindi kirefu kutoka Uingereza.

Necker island before the stormHaki miliki ya pichaVIRGIN
Image captionKisiwa cha Necker kabla ya kimbunga

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi