Uchaguzi Norway unanukia
Utabiri rasmi kuhusiana na uchaguzi wa bunge la Norway unaonyesha kuwa zinaelekea ukingoni huku vyama viwili vikichuana vikali , kati ya chama kikuu chenye mrengo wa kati kulia na kile cha mrengo wa kushoto.
Muungano wa kihafidhina wa Bi Erna Solberg unawania nafasi ya kurejea madarakani kwa kipindi cha pili.Endapo atafanikiwa atakuwa ni mwanamke wa kwanza kutoka chama cha mrengo wa kulia katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kuchaguliwa katika nafasi ya waziri mkuu.
Chama cha upinzani cha Labour kinaonekana kutetea nafasi yake ipasavyo kama chama kikuu katika bunge la nchi hiyo.
Kampeni za uchuzi huo mkuu zimelenga na kuzungumzia vilivyo suala la kodi, pamoja na kupunguzwa kwa ushuru kwa watunga sera ili kuongeza ukuaji wa uchumi, wakati chama cha Labour chenyewe kimejikita katika ahadi ya kuboresha huduma za umma.
Bi Solberg ametawala katika ushirika na chama cha kupambana na wahamiaji .
Comments
Post a Comment