Kyle Edmund ang'ara dhidi ya Tomic - Cheng'du China
Muingereza Kyle Edmund akiwa amerejea dimbani baada ya maumivu amefanikiwa kumshinda Bernard Tomic wa Australia katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Tenisi ya Cheng'du , China.
Mshindi huyo wa nafasi ya 46 Duniani Edmund amemshinda mpinzani wake Tomic kwa seti 6-4 6-2.Leo jumatano Peter Gojozyk anachuana na Leonardo Mayer, Yuichi Sugita dhidi ya Thiago Monteiro, Dusan Lajovic na Albert Ramos, Borna Coric anacheza na Guido Pella, Julio Peralta anachuana na Michael Venus.
Comments
Post a Comment