Kumi washitakiwa maswala ya Rushwa Michezoni
Mamlaka ya serikali ya Marekani imewakamata na kuwashtaki watu kumi kutoka chuo kikuu cha mchezo wa Kikapu nchini humo kwa kosa la kujihushisha na rushwa ya kiwango cha juu.
Miongoni mwao ni pamoja na makocha wanne wa chuo hicho kikuu pamoja na mtendaji mwandamizi kutoka kampuni ya vifaa vya michezo ya Addidas. Uchunguzi wa FBI uliofanyika chini ya Uratibu wa chama cha mchezo wa kikapu pamoja na makocha na wajumbe ambao wamekuwa wakiwapa mafunzo wachezaji wenye vipaji zaidi kuhudhuria mafunzo katika vyuo vingine. Baadhi ya makocha pia walishtakiwa kwa kosa la rushwa kwa kosa la kuwambia wachezaji kusiani na baadhi ya makampuni ambayo yatakuja kufaidika pindi wachezaji hao watakapo kuja kujiunga na ligi kuu ya mchezo wa kikapu marekani NBA.
Comments
Post a Comment