Morgan Tsvangirai apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu
Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.
Wafuasi wa chama chake cha MDC, wanasema hali yake siyo mbaya sana, na inatokana na kujituma sana.
Mwaka jana, Bwana Tsvangirai alipatikana na saratani.
Mwandishi wa BBC nchini Zimbabwe, anasema watu wengi wanauliza, iwapo Bwana Tsvangirai, ni mzima vya kutosha, kuweza kuongoza muungano wa upinzani, dhidi ya Rais Robert Mugabe, katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, ameiongoza Zimbabwe tangu mwaka wa 1980.
Comments
Post a Comment