Tevez namba 1 kwa kulipwa mshahara mkubwa duniani, Kocha kataja sababu za kutomchezesha
Inawezekana taarifa hizi zikakushangaza kwa sababu imekuwa kawaida kwa kuona mchezaji mwenye uwezo mkubwa duniani akilipwa mshahara mkubwa, taarifa zilizoripotiwa kutoka China zinaeleza kuwa Carlos Tevezambaye ni mchezaji namba moja duniani kwa kulipwa mshahara mkubwa kocha mpya havutiwi nae.
Kocha mpya wa club ya Shanghai Shenhu ya China Wu Jingui havutiwi na uwezo wa Carlos Tevez na ameanza kumuweka benchi, kitendo ambacho wengi wanahisi staa huyo atarudi tena kwao Argentina katika dirisha la usajili la January baada ya kocha wao mpya kuonesha kutohitaji huduma yake.
“Kwa sasa siwezi kumchezesha kwa sababu hayupo fiti physically, hayuko fiti kucheza, amezidi uzito, kama kwa kiasi kikubwa huwezi kucheza kwa kiwango hakuna point au ulazima wa mimi kukupanga, nimefundisha mastaa wengi wa kubwa lakini sikuwahi kuwapanga kwa sababu ya majina yao tu”>>>Wu Jingui
Tevez ambaye analipwa mshahara wa zaidi ya pound 600,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 1.8 kwa wiki na club yake ya Shanghai, ameifungia timu hiyo magoli mawili katika game 15 na hivi karibuni alicheza na kuzomewa na mashabiki timu yake ikipoteza kwa magoli 2-1 , Tevez amerudi uwanjani baada ya kupona jeraha lake la mguu.
Kama humfahamu vizuri Carlos Tevez amewahi kuvichezea vilabu kadhaa barani Ulaya kama Man United, Man City vya England na club ya Juventus ya Italia na baadae akarudi kwao Argentina kuichezea timu yake ya utotoni ya Bocca Junior kabla ya December 2016 kwenda Shanghai.
Comments
Post a Comment