Rodriguez awika mechi yake ya kwanza Bayern Munich

James Rodriguez


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

James Rodriguez alifunga bao moja na kusaidia ufungaji wa mengine mawili alipoanza mechi yake ya kwanza Bundesliga katika klabu yake mpya ya Bayern Munich.
Aliwasaidia kulaza FC Schalke 04 3-0.
Rodriguez, ambaye yuko Bayern kwa mkono kutoka Real Madrid ya Uhispania, alifungia Bayern bao lao la pili mechi hiyo.
Katika bao la kwanza, beki Naldo alinawa krosi ya mchezaji huyo wa Colombia na kuwazawadi Bayern mkwaju wa penalti ambao ulifungwa na iRobert Lewandowski.
Rodriguez aliwachenga mabeki wawili kabla ya kuupaisha mpira juu ya safu ya ulinzi ya Schalke na Arturo Vidal akafunga.
James Rodriguez

Image captionRodriguez (pili kushoto) alihamia Real Madrid kutoka Monaco kwa £71m mwaka 2014

Sven Ulreich alikuwa analinda lango la Bayern baada ya taarifa kutokea mapema jana kwamba Manuel Neuer atakwua nje ya uwanja hadi Januari baada ya kufanyiwa upasuaji mguu wake wa kushoto.
Vijana hao wa Carlo Ancelotti wanaongoza ligi baada ya kushinda mechi nne kati ya tano walizocheza.
Borussia Dortmund hata hivyo wanaweza kuwapita iwapo watalaza Hamburg Jumatano.
Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi ambaye yuko kwa mkopo Wolfsburg aliwafungia bao lake la kwanza na kuwasiadia kutoka sare 1-1 nyumbani dhidi ya Werder Bremen.
Borussia Monchengladbach nao walilaza Stuttgart 2-0.
Augsburg waliendelea na mwanzo wao mzuri baada ya bao la dakika ya nne la Michael Gregoritsch kuwapa ushindi wa 1-0 dhidi ya RB Leipzig waliomaliza wa pili msimu uliopita.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi