Messi afungia Barcelona mabao manne mechi moja La Liga

Lionel Messi



Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Lionel Messi alifunga mabao manne na kuwasiadia viongozi wa La Liga Barcelona kuendeleza rekodi yao ya kushinda mechi zote msimu huu kwa kuandikisha ushindi mkubwa dhidi ya Eibar.
Messi alifunga mkwaju wa penalti na kuwaweka wenyeji hao kifua mbele kabla ya Paulinho kufunga la pili kwa kichwa.
Denis Suarez kisha alifunga kutoka kwa mpira wa kudunda lakini Sergi Enrich akawakombolewa Eibar bao moja na kufanya mambo kuwa 3-1.
Messi alifunga mabao mawili katika muda wa dakika moja kabla ya kubadilishana pasi murua na Aleix Vidal na kufunga bao lake la nne dakika za mwisho kwenye mechi hiyo.
Ushindi huo unawaweka Barcelona uongozini wakiwa na alama 15, alama tano mbele ya Sevilla walio wa pili ingawa Barca wamecheza bao moja zaidi.
Messi kwa mara nyingine anaonekana kung'aa mbele ya wavu.
Lionel Messi


Image captionMessi amefunga mabao 12 mashindano yote msimu huu

Mshambuliaji huyo wa Argentina amefunga mabao tisa mechi zake nne za karibuni La Liga.
Bao lake la nne Jumanne limefikisha 301 idadi ya mabao ambayo amefunga Nou Camp katika kipindi cha miaka 13.
Simone Zaza


Image captionZaza alicheza mechi nane akiwa West Ham kwa mkpo kutoka Juventus msimu uliopita. Hakufunga hata bao moja.

Mshambuliaji wa zamani wa West Ham Simone Zaza naye alifunga mabao matatu katika kipindi cha dakika tisa na kuwasaidia Valencia kulaza Malaga 5-0.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi