Uchambuzi: Uamuzi wa Mahakama Kuu Kenya unaupa motisha upinzani
Wakati jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Kenya David Maraga alipo batilisha matokeo ya uchaguzi wa Kenya alikuwa amesema kuwa alibaini "hitilafu na ukiukaji wa sheria " katika mchakato wa uchaguzi.
Uamuzi wa leo uliainisha madai yote hayo kwa kina. Mahakama imeishutumu Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo (IEBC) kwa kushindwa kufuata sheria katika utendaji wake.
Shutuma hiyo inakuja wakati IEBC ikikabiliwa na mzozo wa imani kwa raia.
Mahakama imeupatia upinzani silaha zaidi ya kushinikiza kufutwa kazi kwa maafisa wa tume ya IEBC na mageuzi katika mifumo uchaguzi kabla ya uchaguzi wa marudio.
Majaji wameafiki hoja ya upinzani kwamba kampuni iliyochapisha karatasi za kupigia kura, kwamba baadhi ya karatasi hizo hazikuwa na ishara za usalama.
Muungano wa upinzani Nasa wanataka IEBC kuitafuta kampuni nyingine ya kuchapisha karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio.
Hii inamaanisha kwamba mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati anakabiliwa na shinikizo kubwa ikubadili kikosi chake na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi, suala ambalo linaonekana haliwezekani.
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Uhuru Ruto, ambao hawakuficha ukosoaji wao kwa majaji, walijibu pia. Rais alimtaja Jaji Maraga kama muhuni ''mkora'' na akatishia kukabiliana naye baada ya uchaguzi wa marudio.
Bwana Maraga alijibu tisho hilo kwa njia yaisiyo ya woga.
Alisema atatetea utawala wa kisheria licha ya "vitisho".
Comments
Post a Comment