Sharapova atupwa nje michuano ya Kremlin
Maria Sharapova ametupwa nje ya michuano ya kombe la Kremlin katika hatua ya kwanza siku mbili baada ya kushinda kikombe ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 2015.
Sharapova raia wa Urusi mwenye miaka 30 amepoteza kwa seti 7-6 (7-3) 6-4 mbele ya Magdalena Rybarikova wa Slovakia ikiwa ni mchezo wake wa tano ndani ya siku saba.
Ilikuwa pia ni mchezo wa kwanza kwa Sharapova mjini Moscow ndani ya kipindi cha miaka 10.
Ushindi wake katika michuano ya China ulikuwa wa kwanza kwa kipindi cha miezi 15 alipokuwa akitumikia adhabu ya kukaa nje ya mchezo huo kutokana na kutumia dawa zilizokataliwa michezoni.
Sharapova anayeshikilia nafasi ya 57 duniani alipewa kadi maalumu ya mualiko wa kushiriki michuano ya Kremlin ikiwa ni michuano ya nane kushiriki tokea alipomaliza adhabu yake mwezi April.
Comments
Post a Comment