Viongozi 12 kukutana ili kujadili migogoro inayoendelea Afrika

Viongozi wa bara la Afrika katika mkutano wa awali nchini Ethiopia


Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionViongozi wa bara la Afrika katika mkutano wa awali nchini Ethiopia

Viongozi kutoka mataifa 12 ya bara Afrika wanatarajiwa kukutana katika mji mkuu wa Congo Brazzaville kwa mkutano wa siku mbili utakaoangazia maswala tata yanayoligubika bara hili.
Mkutano huo wa kimataifa katika eneo la maziwa makuu utazungumzia migogoro kadhaa ikiwemo ile katika taifa la jamhuri ya Afrika ya kati ,Sudan Kusini, Burundi na jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC .
Muhariri wa BBC barani Afrika anasema kiwango kikubwa cha fedha , rasli mali na wataalam zimetumiwa bila mafanikio katika kutataua mizozo hapo awali.
Viongozi hao wa kisiasa kutoka Angola Burundi Jamhuri ya Afrika ya kati CAR ,Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo DRC , Kenya , Rwanda, Sudan , Sudan Kusini , Tanzania, Uganda na Zambia hawajakutana katika mkutano wa kiwango kama hicho tangu mwezi Juni 2016.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi