Wanawake kuruhusiwa kuingia viwanja vya michezo Saudi Arabia
Saudi Arabia itawaruhusu wanawake kuhudhuria michezo katika viwanga vya michezo kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka ujao.
Familia zitaweza kuingia kwenye viwanja vitatu vya michezo vya - Riyadh, Jeddah na Dammam.
Ni hatua nyingine ya kuwapa wanawaka wa Saudi Arabia uhuru zaidi, ambao kawaida hukumbwa na ubaguzi wa kijinsia na baada ya kuendolewa marufuku ya kuendesha magari.
Mfalme Mohammed bin Salman yuko katika harakati kubwa kuifanya Saudi Arabia kuwa nchi ya kisasa na kuboresha uchumi.
Mabadiliko hayo yanaambatana na mipango mikubwa ya mabadiliko yaliyotangazwa na mfalme huyo wa umri wa miaka 32 kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa taifa hilo linalotegemea mafuta, yanayojulikana kama maoni ya mwaka 2030.
Mwezi uliopita amri ya kifalme ilisema kuwa wanawake wanaweza kuendesha magari kwa mara ya kwanza kuanzia mwezi Juni mwaka ujao. Warsha zinafanywa na sinema zinatarajiwa kurejeshwa tena.
Siku ya Jumatano Prince Mohammed alisema kurejeshwa kwa uislamu wa wastani ni kiungo muhimu cha kuifanya nchi kuwa ya kisasa.
Alisema kuwa asilimia 70 ya watu nchini Saudi Arabia wana umri wa chini ya miaka 30 na alisema kuwa wanahitaji maisha ambayo yanastahili dini.
Lakini wadadisi wanasema mipango haitakosa pingamiza.
Wanawake nchini Saudi Arabia bado ni lazima wafuate mitindo ya mavazi na wasikuwe na mahusiano na wanaume wasiostahili.
Comments
Post a Comment