Generali Constantine Chiwenga aliyechukua mamlaka ya rais Mugabe

Generali Chiwenga


Haki miliki ya pichaAFP
Image captionGenerali Chiwenga alikuwa na mchango mkubwa katika kuendelea kumuweka madarakani Bwana Mugabe baada ya kushindwa katika uchaguzi dhidi ya mpinzani wake mkuu , Morgan Constantine Tsvangirai

Generali Constantine Chiwenga, mwenye umri wa miaka 61, anasifiwa kama mkombozi wa kisiasa baada ya kuongoza mchakato wa jeshi wa kuchukua mamlaka nchini Zimbabwe, 
Hata hivyo anakabiliwa na vikwazo vya Muunga wa Ulaya na Marekani kwa nafasi yake katika mateso dhidi ya upinzani na kuchukuliwa kwa mashamba ya wazungu.
Raia wa Zimbabwe waliingia mitaani Jumapili kudai rais Robert Mugabe ajiuzulu huku wakiwa wameshikulia mabango yaliyoandikwa: " jeshi la Zimbabwe-sauti ya watu."
Pastor Patrick Mugadza, alifanyiwa mateso na polisi mwenzi wa January mwaka huu kwa kutabiri kuwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93- atakufa katika kipindi cha miezi tisa ijayo , na kwamba Mugabe alitaka kumpatia cheo cha Ujenerali mwanae wa kiume .

Generali ChiwengaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionGenerali Chiwenga aliingilia kati kumaliza mateso ya kiuchumi wanayo yapata raia wa Zimbabwe

Hata hivyo , Generali Chiwenga alikuwa na mchango mkubwa katika kuendelea kumuweka madarakani Bwana Mugabe baada ya kushindwa katika uchaguzi dhidi ya mpinzani wake mkuu , Morgan Tsvangirai wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC), mamo mwaka 2008, huku kukiwa na ripoti kwamba Bwana Mugabe alikuwa anajiandaa kukubali kushindwa.
"alimuambia Mugabe: 'hatuwezi kushindwa katika uchaguzi. Hatuwezi kukikabidhi chama cha MDC mamlaka.
Tutawanyang'anya ushindi ," Mhariri wa Jarida lenye makao yake nchini Uingereza la Africa confidential magazine Patrick Smith aliiambia BBC, na kuongeza kuwa aliendesha operesheni na Emmerson Mnangagwa, kwa hivyo Generali Chiwenga anajaribu kumuweka mamlakani kama mrithi wa Bwana Mugabe.
" Ni Marafiki wakubwa ,"Alisema Bwana Smith.

Mfuasi huyu wa upinzani ni mmoja wa maelfu waliosema kuwa nyumba zao zilishambuliwa na wanamgambo wanaounga mkono chama cha -Zanu-PFHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMfuasi huyu wa upinzani ni mmoja wa maelfu waliosema kuwa nyumba zao zilishambuliwa na wanamgambo wanaounga mkono chama cha -Zanu-PF

Baada ya kucheleweshwa kwa matokeao kwa muda mrefu, matokeo rasmi yalitangazwa yakionyesha kuwa Bwana Tsvangirai hakupata 50% aliyohitaji kupata ili ashinde kwa hivyo awamu ya pili ya uchaguzi inapaswa kufanywa.
Kabla ya uchaguzi wa marudio , wanamgambo wanaounga mkono chama tawala cha -Zanu-PF wakiungwa mkono na wanajeshi waliwashambulia wafuasi wa upinzani kote nchini Zimbabwe, kwa kuwapiga, kuwabaka na kuwauwa. Bwana Tsvangirai akalazimika kujiondoa katika awamu ya pili ya urais na Mugabe akabakia mamlakani.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi