Mugabe akabiliwa na kura bunge ya kutokuwa na imani nae

Robert Mugabe


Haki miliki ya pichaEPA/THE HERALD
Image captionRais Mugabe anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa umma na chama chake cha Zanu-PF

Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.
Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.
Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''.
Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliyeuhamishoni karibuni.
Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae. 
Jumapili , licha ya shinikizo kubwa Bwana Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuma yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi