Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 20.11.2017

Mshambuliaji wa Uingereza na Tottenham Harry Kane, 24,


Image captionMshambuliaji wa Uingereza na Tottenham Harry Kane, 24,

Manchester City itashindana na Liverpool kumununua beki wa Southampton na Uholanzi Virgil van Dijk, 26, katika dirisha la uhamisho la Januari.{Daily Mirror}.
City pia inataka kumsajili kiungo wa kati wa Schalke na Ujerumani Leon Goretzka ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu na amewavutia Arsenal, Liverpool na Chelsea (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Uingereza na Tottenham Harry Kane, 24, anasema kuwa anapanga kuichezea Tottenham kwa kipindi chote cha mchezo wake kilichosalia (London Evening Standard)

Daniel Sturridge
Image captionDaniel Sturridge

Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 28, yuko tayari kuondoka Liverpool ili kuweza kuchezeshwa na kuweza kuhifadhi nafasi yake katika timu ya Uingereza. (Daily Mirror)
Barcelona inapanga kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil na inaweza kumuuza mchezaji wa Ureno Andre Gomes badala yake (Don Balon - in Spanish)
Nahodha wa Paris St-Germain Thiago Silva anasema kuwa amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, na anatumai mchezaji mwenza wa Brazil atajiunga na klabu hiyo.

Royad Mahrez
Image captionRoyad Mahrez

Klabu ya Manchester City huenda ikamnunua winga wa Leicester Riyad Mahrez baada ya kiungo wa kati wa Barcelona Lionel Messi kukataa raia huyo wa Algeria ajiunge na Barcelona (Don Balon - in Spanish)
Liverpool na Tottenham zinamtazama kinda wa Sheffield United's na mchezaji wa Wales David Brooks. (Daily Express)
Bournemouth inajiandaa kumununua beki wa Reading mwenye umri wa miaka 19 Omar Richards. (Sun)

Mshambuliaji wa Switzerland Xherdan Shaqiri
Image captionMshambuliaji wa Switzerland Xherdan Shaqiri

Mshambuliaji wa Switzerland Xherdan Shaqiri ana thamani ya juu sana ikilinganishwa na kiwango cha £12m ambacho Stoke kilimlipia takriban miaka miwili iliopita ,kulingana na mkufunzi Mark Hughes says. (Stoke Sentinel)
Arsenal itawalipa Borussia Dortmund takriban £1.8m ili kumuajiri afisa anayesaka wachezaji wazuri Sven Mislintat anayejulikana kama 'Diamond Eye' - kuwa mkuu wa usajili wa wachezaji. (Sport Bild via Sun)

Joachim Low, 57,
Image captionJoachim Low, 57,

Sio rahisi kwa Real Madrid kumsajili kocha raia wa Ujerumani Joachim Low, 57, iwapo watamfuta kazi mkufunzi Zinedine Zidane. (Daily Express)
Refa wa zamani katika ligi ya Uingereza Mark Clattenburg anasema kuwa beki Vincent Kompany wa Manchester City alifaa kupewa kadi nyekundi kwa kumchezea visivyo mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy huku mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse akiadhibiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kudanganya baada ya kushinda penalti dhidi ya Crystal Palace . (Times - subscription required)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anasema kuwa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 24, lazima aonyesha mchezo mzuri kwa miaka 10 ama 15 ili kuweza kufananishwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool Steve Gerrard(Daily Star)

Anthony Martial na Marcus Rashford
Image captionAnthony Martial na Marcus Rashford

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amefichua kwamba huwachezeshi pamoja Anthony Martial na Marcus Rashford kwa sababu mchezo wao unafanana (Independent)
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 36, anasema kuwa iwapo watu wangejua kuhusu jereha lake, wangeshangaa kwamba anacheza , kufuatia kurudi uwanjani kwa kile kilichotajwa kuwa jeraha la goti alilopata mwezi Aprili(Guardian)
Mshambuliaji wa huyo wa zamani wa Sweden anaamini kwamba Manchester United inaweza kushindana na wapinzani wao wa jadi Manchester City kushinda taji la Uingereza.. (Daily Mail)

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi