Mkuu wa zamani wa soka Amerika Kusini kushitakiwa kwa rushwa
Jaji mmoja nchini Paraguay ameruhusu upelelezi kuanza kwa mkuu wa zamani wa shirikisho la soka la Amerika ya Kusini Nicolas Leoz kwa tuhuma za rushwa.
Leoz ni mmoja ya watuhumiwa wakubwa wa rushwa waliotajwa na mahakama moja nchini Marekani.
Bosi huyo wa zamani wa FIFA amekuwa chini ya uangalizi mkali nyumbani kwake Asuncion Paraguay.
Anatuhumiwa pia kupokea rushwa ili kuiruhusu Qatar kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.
Leoz anasema tuhuma hizo ni za uongo huku mwanasheria wake akiapa kukata rufaa.
Comments
Post a Comment