Posts

Image
Kwa wale ambao walikuwa hawaifahamu karafuu ndo hii hapa Namna karafuu inavyokaa kwenye mmea wake. K arafuu ni tumba lililokauka la maua yasiyofunguka yanayopatikana kutoka mti mzuri wa kati na kijani. Mti huu una shina lilinyooka na hukua kufikia kimo cha mita 10 hadi 12. Karafuu imekuwa ikitumiwa India na Uchina kwa zaidi ya kwa zaidi ya miaka 2000 kama kiungo cha kulinda kuoza meno na kutoa harufu mbaya yaaani pumzi mbaya. Mti wa karafuu una asili ya visiwa vya Molluca. Wachina walipata kiungo hiki mnamo karne ya 3 K.K (Kabla ya Kuzaliwa Kristo). Karafuu ziliingizwa Alexandria mapema mwaka 176 B.K (Baada ya Kuzaliwa Kristo). Mnamo karne ya 4 hivi B.K ulijulikana vema katika meditarrania na katika karne ya 8 ulaya nzima. Inasemekana huko visiwa vya pemba na unguja (Zanzibar) karafuu ililetwa na sultani mmoja ikiwa imewekwa kwenye fimbo ya mwanzi leo hii Zanzibar ndio mzalishaji anayeongoza kwa kuzalisha karafuu nyingi ulimwenguni. Sifa ilizonazo karafuu ni wang...
JE? UNAFAFAHAMU FAIDA YA MAFUTA YA UBUYU KWA  NGOZI YAKO. Mafuta ya ubuyu yamefanyiwa uchunguzi kwa muda mrefu na watafiti mbalimbali na kugundua kuwa mafuta ya ubuyu yana vitamini nyingi zinzoitajika katika kuirutubisha ngozi.wanawake wengi wa ulaya na afrika wamebadilisha mtindo wa maisha na kuanza kutumia bidhaa asilia kama mafuta ya ubuyu ambayo pia ni dawa ya jenga ngozi iliyoharibika mikorogo na vipodozi vyenye kemikali  kali.pian  uondoa harara,chunusi na fangasi usoni na mwilini lwa  ujumla.Pia  mafuta haya yanauwezo mkubwa wa kuikinga ngozi dhidi ya miale ya jua hata alibino wa jinsia yoyote wanashauriwa kutumia mafuta haya kulinda ngozi  zao.Siku  za hivi karibuni kumekuwepo na muamko mkubwa kwa wanawake wa afrika kutumia mafuta ya ubuyu baada ya kufahamu faida yake.Matumizi ya mafuta haya ni kwa kupakaa mwilini bila kujali muda kutegemea na muhusika au mtumiaji .
Image
faida ya ubuyu kwa mwili wa binadamu. Muonekano wa ubuyu uliopo kwenye kasha lake na vipeke vilivyotolewa unga wake. Inaaminika na baadhi ya watu kuwa ubuyu ni tunda lisilokuwa na thamani sana, kwani hata mtu akiwa anafanya biashara ya kuuza ubuyu hudharaulika, pengine ni kutokana na watoto na watu wa hali ya chini kupenda kutumia. Lakini habari za hivi karibuni zinatoa taswira tofauti kuhusu tunda hili. Taswira hii inaweza kabisa kubadilisha mtazamo wa baadhi ya watu waliokua wakilidharau tunda hili. Hivi karibuni Jumuiya ya Ulaya (EU) imeidhinisha kuingizwa kwa tunda hili barani humo kama tunda la kibiashara baada ya kampuni ya PhytoTrade Africa kupewa kibali cha kuingiza tunda hilo kutoka Afrika. Kampuni hiyo hivi sasa imeruhusiwa kuingiza ubuyu katika bara hilo na kutumiwa na wananchi wake kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuchanganya na vyakula mbalimbali vya nafaka ili kuongeza virutubisho. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, Ubuyu una kiwango kikubwa cha Vitamin C ...
Image
Muonekano wa ubuyu unaofaa kutengeneza juisi ya ubuyu. Maajabu ya juisi ya Ubuyu Unga wa ubuyu  unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa. 1. Inaelezwa kuwa  unga wa ubuyu  una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa. 2.  Ubuyu  una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi! 3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini 4. Ina virutubisho vya kulinda mwili 5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika  kuondoa sumu mwilini  na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye  afya  zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2. 6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C 7. Huongeza nuru ya macho 8. ...

mwanamke aishi na wanaume wawili kiunyumba miaka nane bila kutambuana.

Image
MWANAMKE AISHI KINYUMBA NA WANAUME WAWILI KWA MIAKA NANE BILA KUTAMBUANA MBEYA Juliana Josia(22)kushoto anaedaiwa kuishi na wanaume wanaume wawili kwa zaidi ya miaka 8 bila kutambuana akiwa na Mume wake halisi Rogers ofisini kwa mtendaji Juliana Josia(22)kushoto akiwa na barozi Dinde  Bwana Rogers akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa kwenda kituo cha polisi Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juliana Josia(22)amezua utata hivi karibuni baada ya kugunduliwa akishi na wanaume wawili kwa muda wa miaka minane bila wanaume hao wawili  kujitambua. Hayo yalibainika katika kituo cha Polisi Kati Jijini Mbeya baada ya Mwanamke huyo kudai kuporwa mtoto mgogoni jinsi ya kike mwenye umri wa miaka miwili eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya kutishiwa na Biton Bomani Mwashilindi mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya. Juliana alidai kuporwa mtoto na Biton Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi alipokuwa akielekea soko ...
Image
TAARIFA YA TUKIO LILILOTOKEA UBUNGO PLAZA KATIKA MKUTANO WA MWALIMU NYERERE FOUNDATION  Mkutano ulifanyika kuanzia saa 1520hrs ukiwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu mh. Joseph Sinde Warioba. Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na ITV na maudhui yake kimtazamo ulilenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya tume ya Warioba na ile ya Mh. Sitta na tume yake. Baada ya Mh. Warioba kuelezea kwamba Muungano sio tunu ila ni urithi ndipo wakereketwa wa upande wa Mh. Sitta walipoinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya katiba ya Mh. Sitta ambayo wao wameshaikubali? Baada ya mabango yale kuinuliwa yakazua tafrani ambapo walishauriwa kutoyainua kwa sababu haukuwa mkutano wa kisiasa na wakanyang’anywa na kuyachana ndipo vurugu/kashfa/matusi yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha kushikana, kusukumana na kurushiana viti. Katika t...