Posts

Matokeo ya urais ya wagombea wote wanane

Image
mepakiwa mnamo 8:40 Kulikuwa na wagombea wanane katika kinyang'anyiro cha urais nchini Kenya. Matokeo kamili yalikuwa kama ifuatavyo: Ekuru Aukot 27,311 (0.18) Abduba Dida 38,093 (0.25) Cyrus Jirongo 11,705 (0.08) Japheth Kaluyu 16,482 (0.11) Uhuru Kenyatta 8,203,290 (54.27) Michael Wainaina 13,257 (0.09) Joseph Nyagah 42,259 (0.28) Raila Odinga 6,762,224 (44.74) Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.2 na pia akapata angalau asilimia 25 ya kura katika kaunti 35. Mshindi wa urais huhitajika kupata asilimia 50 ya kura na kura moja zaidi, pamoja na angalau asilimia 25 katika kaunti 24. Baada ya kutangazwa mshindi, alitoa wito kwa mpinzani wake Raila Odinga, ambaye muungano wake uliyakataa matokeo, aungane naye kufanya kazi kwa maslahi ya taifa. ""Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamo...

Uchaguzi Kenya 2017: Hali baada ya Kenyatta kutangazwa mshind

Image
   Rais Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais Ijumaa usiku baada ya kupata kura 8, 203, 290 sawa na       asilimia 54.2 zilizopigwa Mgombea wa upinzani Raila Odinga alipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.7 Baada ya matangazo, visa vya maandamano viliripotiwa katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani, mfano Kisumu, Homa Bay na Migori magharibi mwa nchi hiyo Kulitokea pia visa vya maandamano na polisi kufyatua gesi ya kutoza machozi katika baadhi ya mitaa jijini Nairobi      Hali ya kawaida yarejea Garissa Imepakiwa mnamo 9:33 Hali ya kawaida imeanza kurejea mjini Garissa siku moja baada ya matokeo ya uchaguzi wa urais kutangazwa. Sehemu ya soko kuu mjini humo iliteketezwa Jumatano wakati wa ghasia kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa ugavana. Lakini jana na leo hali imekuwa tulivu. Mwandishi wetu Bashkas Jugsodaay amepiga picha hizi za wananchi wakiendelea na shughuli zao za kawaida leo asubuhi.

Vita ya Diamond Platnumz na Alikiba Kuamuliwa Nigeria

Image
Jana usiku majina ya wasanii waliochaguliwa kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za AFRIMA 2017 yametangazwa ambapo kwenye kipengele cha Msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki mahasimu Diamond Platnumz na Alikiba wamekutana tena kwenye kipengele hicho na ndiyo Wasanii pekee waliofanikiwa kuingia kwenye kipengele hicho. Wasanii wengine kutoka Tanzania waliotajwa kwenye tuzo hizo ni Lady Jaydee, Nandy na Vanessa Mdee wote wapo kwenye kipengele cha msanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki. Upigaji kura wa Tuzo hizo utaanza Tarehe 21 Agosti mwaka huu na zitatolewa tarehe 12 mwezi Novemba huko Lagos nchini Nigeria, Tazama Orodha kamili ya tuzo za AFRIMA 2017 hapa chini.

Waziri Mwijage Acharuka.......Avifunga Viwanda 10 kwa Kushndwa Kuendelezwa

Image
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, amesema serikali imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya kutwaa viwanda walivyopewa wawekezaji na kushindwa kuviendeleza huku viwanda vingine vikiwa chini ya uangalizi wa muda Waziri Mwijage amesema hayo jana Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao kilichojumuisha wawakilishi wa Wizara za Fedha, Tamisemi na Wizara ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu. Amevitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha korosho Lindi, Mgodi wa Pugu Kaolin, Mkata Saw Mills Ltd, Manawa Ginnery Co Ltd, Kiwanda cha Chai Dabaga, Tembo Chipboard Ltd, Kiwanda cha Nguo cha Kilimanjaro, Mang’ula Mechanical and Machine Tools co. Ltd na Polysacks cha Dar es Salaam. Aidha, Mhe. Mwijage amesema serikali ambayo awali ilibinafsisha mashirika 341 ya umma ambayo yalijumuisha viwanda, mashamba, makampuni ya biashara, mahoteli na makampuni ya usafirishaji lakini kati ...

Tume ya uchaguzi Kenya yashangazwa na matokeo ya upinzani

Tume ya Uchaguzi ya Kenya imesema ni mapema na ni kinyume cha sheria kwa mgombea wa upinzani Raila Odinga kujitangazia kuwa ameshinda uchaguzi wa Kenya. Alhamisi, muungano wa upinzani wa NASA ulichapisha matokeo ambayo yanaonyesha kuwa Raila Odinga amemshinda Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, ambapo pia waliitaka tume ya uchaguzi imtangaze Odinga kuwa ndiye Rais mteule. Hata hivyo matokeo ya awali hadi sasa yaliyotangazwa na tume hiyo yanaonyesha Rais wa sasa Uhuru Kenyatta bado anaongoza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga. Mwandishi wetu Anne Soy alifanya mahojiano na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati. Kwanza alimuuliza, je tume hiyo imepokea barua yoyote kutoka upinzani?

Mfumuko wa bei washuka nchini.

Image
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini kwa kipindi cha Julai mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwapo mwezi Juni mwaka huu hali inayomaanishakasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa imepungua. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo, amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa kipindi cha Julai mwaka huu kumechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2017 ikilinganishwa na bei za Juni 2016. “Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na nyama, kwa asilimia 16.6, bilinganya (10.6), vitunguu (13.2), karoti (16.9) na viazi mviringo (13.5)"  amesema. Aidha ameeleza kuwa Shilingi ya Tanzania imezidi kuimarika ambapo uwezo wa Shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma ulifikia Shilingi 91 na senti 87 kipindi cha Julai 2017 ikilinganishwa na shilingi 91 na senti 66 ilivyo...

Korea Kaskazini: Tuna mpango wa kushambulia kisiwa cha Marekani cha Guam siku chache zinazokuja

Image
Haki miliki ya picha Image caption Korea Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam Korea Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni huku majibizano ya kivita kati yake na Marekani yakiendelea. Vyombo vya habari vilisema kuwa makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan na kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Guam ikiwa mpango huo utaidhinishwa na Kim Jong-un. Korea ilipuuzna onyo la Donald Trump kuwa itashambuliwa vikali. Marekanai imeionya Korea Kaskazini ikisema kuwa vitendo vyake vinamaanisha kuwa huo utakuwa mwisho wa utawala wa nchi hiyo. Image caption Kisiwa hicho kilicho bahari ya Pacific cha Guam ndiko ziliko kambi za jeshi za Marekani na watu 163,000 Waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis alisema kuwa Korea Kaskazini itashindwa vibaya ikiwa itaingia vitani na Marekani na washirika wake. Korea Kaskazini ilitangaza si...