Posts

Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini

Image
Image caption Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu. Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu. Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana. Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua. Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban. Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa. Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza. Wachunguzi wa visa vya uh...

Wataalumu waonya kuhusu kuundwa roboti zinazoweza kuua

Image
Haki miliki ya picha Image caption Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha. Zaidi ya wataalamu 100 wa teknolojia ya roboti wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ili kuzuia kundwa wa roboti zinazoweza kuua. Kwenye barua kwa Umoaj wa Mataifa, wataalamu wa masuala ya teknolojia akiwemo tajiri Elon Musk, wameonya kuwa hatua hiyo itasababisha kuwepo kwa vita vitakavyohusisha roboti. Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha. "Wakati zitaundwa, zitawezesha vita kupiganwa kwa kiwango kingine cha juu na kwa haraka zaidi kuliko vile binadamu hufanya." barua hiyo ilisema. "Hizi zitakuwa silaha za ugaidi, silaha ambazo magaidi watatumia dhidi wa watu wasio na hatia, na silaha ambazo zitadukuliwa kuhudumu kwa njia ambayo sio nzuri." iliongeza Mwaka 2015 zaidi ya wataalamu 1,000 na watafiti waliandika barua w...

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

Image
Haki miliki ya picha Image caption Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto. Marekani na Korea Kusini wanafanya mazoezi ya kila mwaka ya jeshi, ambayo mara nyingi huighadhabisha Korea Kaskazini licha ya wito wa kutaka mazoezi hayo yasifanyike. Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilionekana kulegeza kamba baada ya kutisha kuwa itarusha makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, lakini tena ikasema kuwa itafuatilia mienendo ya Marekani. Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto. Haki miliki ya picha Image caption Mazoezi hayo hujumuisha ya ardhini , baharini na angani China na Urusi mwezi Julai zilipendekeza kusitishwa mazoezi ya kijeshi ili nayo Korea Kaskazini iache kuyafanyia majaribio makombora. Marekani inasema kuwa mazoezi hayo yatawahusisha wanajeshi 17,500 wa Marekani na yatadumu kwa kipindi cha siku kumi. 'Kifaa' cha Korea K...

Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore

Image
Haki miliki ya picha Image caption Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa baada ya manowari ya jeshi la Marekani kugongana na meli ya kubeba mafuta pwani mwa Singapore, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani. Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia. Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa wanajeshi inaendelea Ndicho kisa cha pili kikubwa kinachoikumba meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni. Ripoti zinasema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu upande wake mmoja, lakini jeshi la Marekani lilsema kwa inaelea peke yake kwenda bandari ya Singapore. Image caption Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singap...

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Pale Unapohitaji Mkopo Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Nyumba Ya Ndoto Yako.

Image
Nimepewa siku nyingine tena ambayo napaswa niitumie vizuri kwa kadri nitakavyoweza ili iweze kuleta tija kwa maisha yangu binafsi pamoja na maisha ya kizazi hiki ndani ya nchi yetu ya Tanzania. Hii ni zawadi ya pekee ambayo thamani yake hakuna mwanadamu anaweza kuielezea pasipo na shaka ya aina yoyote. Zawadi iliyo kuu kwangu ni uzima na afya njema ambayo Mungu ameendelea kunitunuku hata muda huu ambao umenilazimu niwaambie jambo marafiki na jamaa zangu wa Tanzania. Leo napenda niwakumbushe marafiki ambao wapo kwenye hatua mbalimbali za uwekezaji wa ardhi na majengo ambao wamedhamiria kweli kufikia malengo makuu waliyojiwekea na wana mpango wa kuomba mkopo kupitia taasisi za fedha, Ni jambo jema sana kuzitumia taasisi hizi za fedha kufikia ndoto zetu kwa namna zozote vile itakavyowezekana, hii ni mbinu mojawapo ambayo baadhi ya marafiki zetu hutumia taasisi za fedha kama chanzo saidizi kwenye uwekezaji huu. Changamoto ni kwamba wengi wa marafiki wameshindwa na marafiki wachache n...

Uchaguzi Kenya: Upinzani wawasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Kenyatta

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Odinga anadai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa kumfaa Kenyatta Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance umewasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti. Mawakili wa muungano huo wamewasilisha nyaraka za kesi hiyo na ushahidi katika majengo ya Mahakama ya Juu mjini Nairobi takriban saa moja unusu kabla ya muda ulioruhusiwa kumalizika. Nyaraka na stakabadhi za ushahidi zilizowasilishwa na muungano huo ni za kurasa 9,000. Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa Ijumaa wiki iliyopita ilifaa kuwasilishwa kabla ya saa sita usiku leo, kabla ya kumalizika kwa siku saba tangu kutangazwa kwa matokeo. Mgombea urais wa chama hicho waziri mkuu wa zamani Raila Odinga alikuwa ameapa kutopinga matokeo ya urais tena kortini kabla ya uchaguzi kufanyika na baada ya matokeo kutangazwa. Lakini alibadilisha uamuzi huo na kutangazwa Jumatano wiki h...

ALICHOSEMA WAZIRI UMMY BAADA YA KUFANYA ZIARA KITUO CHA AFYA MATEI, KALAMBO

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka watoa  huduma za afya katika kituo cha afya cha Matei wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili Alisema wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine  vinavyoweza kusababisha  uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua “Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji,” ...