Posts

Rais Kenyatta aitisha maombi kabla ya marudio ya Uchaguzi

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Rais Kenyatta aitisha maombi kabla ya marudio ya Uchaguzi Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nchi itafanya maombi mwisho wa wiki hii kabla ya marudio ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo. Taarifa ya Rais Kenyatta ilikuja baada ya afisa wa cheo ya juu kwenye tume ya uchaguzi nchini Kenya, kukimbia nchi akisema kuwa amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa. Roselyne Akombe aliiambia BBC kuwa marudio ya uchaguzi, hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki. Bw. Kenyatta alisema kuwa wakenya watatumia wikendi kwa maombi na maridhiano kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais ambao utafanyika tarehe 26 mwezi Oktoba. Mpinzani wake mkuu Raila Odinga alijiondoa kutoka kwa uchaguzi huo wiki iliyopita. Hata hivyo Rais Kenyatta hakuzungumzia kujiuzulu kwa Bi Akombe.

Raila Odinga aitisha maandamano ya nchi nzima siku ya uchaguzi Kenya

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Raila Odinga aitisha maandamano siku ya uchaguzi Kenya Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (Nasa), Raila Odinga, amesema kuwa upinzani utafanya maandamano ya nchi nzima tarehe 26 Okotoba. Hii ndiyo siku ya kufanyika marudio ya uchaguzi wa urais. Akihutubia wafuasi wake katika mtaa wa Kamukunji mjini Nairobi leo Jumatano, Bw. Odinga alisema kuwa ataendelea kushikiza Marekebisho katika tume ya uchaguzi ili kuweza kufanyinya uchaguzi ulio wa haki. "Leo tunabadilisha kauli mbiu yetu kutoka "hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi" hadi "hakuna uchaguzi Oktoba," Bw. Odinga alisema huku akisisitiza kuwa amejiondoa kutoka kwa uchaguzi huo. Bw. Odinga alitoa tangazo hilo hata baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuonya kuwa hatua kali zinachukuliwa dhidi ya yeyote ambaye atajaribu kuvuruga marudio ya uchaguzi. Akizungumza eneo la Nanyuki, Rais Kenyatta alilaani visa ambapo maafisa wa IEBC walishambuliwa wakati waki...

Historia mpya aliyoweka Wizkid London

Image
Muimbaji kutokea  Nigeria   Wizkid  anayefanya vizuri na hit single ya wimbo wake  Come Closer  aliyomshirikisha msanii wa Marekani  Drake , ameingia katika historia mpya kwa kuiwekea heshima Afrika baada ya kuweka rekodi  England . Wizkid  akiwa katika show nchini  England  katika jiji la  London  ameandika historia mpya ya kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kuwahi kufanya show  Royal Albert Hall  na kufanikiwa kujaza ukumbi wote. Naambiwa ukumbi wa  Royal Albert Hall  unauwezo wa kuingia mashabiki 5000 na  Wizkid  amefanikiwa kuuza tiketi zote na kukuta mashabiki wakimsubiri ukumbuni kwa zaidi ya saa mbili, kwa mujibu wa waandaaji unaambiwa tiketi za show hiyo zilimalizika siku mbili kabla ya show. Muimbaji kutokea  Nigeria   Wizkid  anayefanya vizuri na hit single ya wimbo wake  Come Closer  aliyomshirikisha msanii ...

PROFESSOR JAY! Baada ya nyumba yake kupitiwa na bomoabomoa

Image
Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Professor Jay’ ni miongoni mwa mahanga wa zoezi la bomoabomoa linaloendelea ambalo linafanywa na TANROADS kuondoa nyumba zilizopo ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro. Baada ya tukio hilo, kupitia Instagram yake, Professor Jay alieleza namna alivyosikitishwa na zoezi hilo lililotokea wakati yupo kwenye majukumu yake ya kibunge kwenye Jimbo la Mikumi. >>>”Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara Tarehe 29/9/ 2017. Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. “(sijawahi kuumia kiasi hiki 😭) Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. ...

Man United yaibana Crystal Palace 4-0

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Kiungo wa kati wa Manchester United Fellaini akiifungua United bao lake la kwanza Klabu ya Manchester United imeonyesha mchezo mzuri na kuweza kuicharaza Crystal Palace 4-0 na hivyobasi kuilazimu klabu hiyo kupoteza mechi yake ya saba msimu huu bila kufunga bao. United ambao hawajapoteza waliongoza baada ya dakika tatu wakati Marcus Rashford alipowachanganya mabeki wa Palace na kutoa pasi nzuri kwa Juan Mata aliyecheka na wavu akiwa umbali wa maguu 10. Bao la pili lilijiri baada ya Ashley Young kupiga krosi ambayo ilifungwa na Marouane Fellaini. Fellaini alifunga bao la pili kupitia kichwa cha karibu kufuatia mkwaju wa adhabu uliopigwa na Rashford mapema katika kipindi cha pili. Romelu Lukaku alifunga bao la nne kunako dakika za lala salama likiwa bao la 11 katika mechi 10 za United, kwa kumaliza krosi iliopigwa na Martial. Matokeo hayo yanaipeleka United katika kilele cha jedwali kwa muda mchache huku Manchester United i...

Kampuni ya China yawanusuru tembo wanne Tanzania

Image
Image caption Ndovu waliokwama wanusuriwa Tanzania Kampuni ya ujenzi ya China Sinohydro imewapeleka wahandisi wake na tingatinga katika eneo la kuhifadhi wanyama pori la Rungwe katikati ya Tanzania ili kuwaokoa tembo watano waliokwama katika shimo. Ndovu wanne wakiwemo watoto wawili waliokolewa lakini ndovu mmoja mkubwa alifariki kutokana na ukosefu wa maji kulingana na chombo cha habari cha China Xinhua. Kulingana na duru kutoka kwa kampuni ya Sinohydro, baadhi ya wakaazi wa manyoni eneo la Singida waliwaita wafanyikazi wa kampuni hiyo kuwasaidia tembo hao yapata kilomita 40 kutoka katika hifadhi hiyo. Saa moja baadaye, waokoaji hao wa China waliwasili katika eneo hilo na kuanza uokoaji baada ya kupata ruhusa kutoka kwa gavana wa eneo hilo na wasimamizi wa hifadhi hiyo. Ndovu wavamia chuo kikuu cha Dodoma Tanzania Kulingana na Xhinua wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa wanyama hao walianguka katika shimo hilo walipokuwa wakitafuta maji. Shimo hilo l...

10 wafariki baada ya ndege ya kijeshi kuanguka DR Congo

Image
Image caption Picha ya ndege ya kijeshi ilioanguka Ndege ya kijeshi imeanguka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwaua abiria wote. Maafisa wa maswala ya angani wamesema kuwa zaidi ya watu 10 wamefariki baada ya ndege hiyo kufeli kupaa vizuri kutoka uwanja wa ndege wa N'djili katika mji mkuu wa Kinshasa na kuanguka katika makaazi ya Nsele. Haijabainika iwapo kuna watu wowote waliouawa ama kujeruhiwa ardhini. Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kinshasa amesema kuwa ndehe hiyo ilikuwa ikibeba mizigo na kwamba haikuwa na abiria wowote. Ripoti nyengine zinasema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuawa.