HALI YA UZALISHAJI UMEME VITUO VYA PANGANI HYDRO SYSTEM VIKO KATIKA HAKLI NZURI; MHANDISI MAHENDA
Mhandisi Mahenda S. Mahenda, Meneja wa Vituo vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro Systems, vinavyohusisha inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Korogwe VITUO vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro Systems , ambayo inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97, viko katika hali nzuri, Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S. Mahenda, amesema Leo Desemba 18, 2017. Hata hivyo amesema, mashine moja kati ya mbili kwenye kituo cha Hale, haifanyi kazi na iko katika matengenezo. “Niwahakikishie tu kwamba matengenezo hayo ambayo bado hayajaanza hayataathiri upatikanaji umeme kwa sababu vyanzo vya umeme vimeongezeka.” Alisema. Akif...