AMPIGA RISASI BABA MKWE WAKE KANISANI


Chanzo cha mwandishi wa habari wa kujitegemea, Elias Mhegera kumpiga risasi baba mkwe wake kanisasni juzi ni hisia kuwa mzazi wa mwanamke huyo ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao miaka 10 iliyopita. Mhegera ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu juzi amekuwa katika mvutano na mke wake ambaye waliachana miaka 10 iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi majira ya saa1:30 asubuhi katika Parokia ya Bikira Maria, Kibangu na kueleza kuwa chanzo ni ugomvi wa kifamilia.
“Adrian Mpande alijeruhiwa bega la kushoto na mtu anayedaiwa kuwa ni mkwe wake. Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa sababu ni mambo ya kifamilia,” alisema Kamanda Kaganda na kuongeza: “Tunaendelea na uchunguzi na kukiwa na umuhimu tutawaeleza kwa uwazi.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Mzee Mpande alipigwa risasi mbili wakati akijiandaa kuingia kanisani kwa ibada juzi Jumapili.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi