Msuva ajitokeza mazoezini na kuaga rasmi viongo wa Yanga SC
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na Yanga SC, Saimon Happygod Msuva amewaaga rasmi wachezaji wenzie wanachama na mashabiki wa klabu hiyo
Kiungo huyo muhimu wa Yanga SC anakwenda nchini Morocco kujiunga na timu ya Difaa al Jadida ambayo imeridhia kuwalipa wana jangwani hao kiasi cha dola 80,000 (Sh milioni 177) kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Akizungumzia suala la kuaga na safari yake Msuva alisema; “Kwanza kabisa nimshukuru mwenyezi mungu kwa kunipatia timu nje ya nchi japo ni ndani ya bara letu ila wenzetu wameendelea (advance) sana kwa hiyo naona ni mahali sahihi kwangu na ni hatua pia kwangu”.
Simon Msuva ameendelea kwa kusema “pili niwashukuru mashabiki wa timu yangu kwa kuwa nami muda wote niliokuwa na timu ya Yanga pia niwashukuru watanzania wote kwa kuendelea kuutambua mchango wangu (support) yao ndio iliyonifikisha hapa nilipo sasa”
“Kikubwa watanzania waniombee ili nikafanikiwe na kusonga mbele zaidi ya hapo”, smesema Simon Msuva.
Naye kocha mkuu wa timu hiyo mzambia George Lwandamina amesema ni hatua kwa mchezaji na taifa kwa ujumla, Msuva ni mchezaji aliyejaaliwa kila kitu akienda akajitunza na kujituma atafika mbali nasi twamuombea mafanikio kwani mafanikio ya Msuva ni mafanikio ya klabu na taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment