Sheria Tano Za Fedha Unazopaswa Kuzijua Na Kuzisimamia Kama Unataka Kuondoka Kwenye Umasikini.

Moja ya vitabu nilivyowahi kusoma kuhusu fedha na nikavielewa na hata kujenga msingi wangu wa kifedha ni kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON. Kitabu hichi kimetoa elimu muhimu sana kuhusu fedha kwa kutumia hadithi ya enzi za utawala wa Babeli. Kitabu hichi kimeeleza kwa kina kuanzia kuongeza kipato, kuweka akiba, kuwekeza, kuondoka kwenye madeni, kulinda utajiri na mengine muhimu. 



Kwenye kitabu hichi, ipo hadithi ya mtu mmoja tajiri, ambaye baada ya kijana wake kufikia umri wa kuweza kujitegemea, alimwita na kumwambia anataka ampime na kuona kama anaweza kurithi mali zake. Na alimpa mfuko wa fedha, pamoja na kitabu cha sheria za fedha, na kumwambia miaka kumi ijayo, arudi kwake na kumwambia amefanya nini na fedha zile. 

Kama ilivyo kwa wengi wanaopata fedha nyingi kwa wakati mmoja, hakuhangaika na zile sheria za fedha, badala yake alianza kutumia fedha zile. Alishauriwa kujihusisha na biashara asizozielewa, mojawapo ikiwa ni kamari na kupoteza fedha zote. Baada ya kubaki hana kitu, ndiyo alikumbuka baba yake alimpa sheria za fedha, akazitafuta na kuanza kuzisoma na kuzifanyia kazi. Miaka kumi baadaye alirudi kwa baba yake akiwa na fedha mara tatu ya alizoepwa, na kumshukuru baba yake kwa sheria zile. 

Sura hii inaanza na maelezo kwamba, mpe mtu achague kati ya fedha ua hekima ya fedha, wengi watakimbilia fedha. Kinachotokea, wanapuuza hekima ya fedha, na kupoteza fedha wanazokuwa wamekimbilia. 

Hivyo kabla ya kutaka kuongeza kipato na hata kufikia utajiri, ni vyema tukajifunza sheria hizi tano muhimu za fedha. Sheria hizi ni za vizazi na vizazi, hazipitwi na wakati. Sheria hizi nimezitoa kwenye kitabu hichi cha THE RICHEST MAN IN BABYLON. Tuzisome na kuziishi maisha yetu yote, tutajenga msingi imara kifedha. 

SHERIA YA KWANZA YA FEDHA; KUJILIPA MWENYEWE. 

Fedha huenda kwa mtu ambaye anatenga siyo chini ya sehemu ya kumi ya kipato chake kwa ajili ya maisha ya badaye kwake na kwa familia yake. 

Hapa ndipo ilipo dhana ya kujilipa wewe mwenyewe kwanza. Kwamba kipato chochote kinachopita kwenye mikono yako, hata kiwe kidogo kiasi gani, hakikisha sehemu ya kumi ya kipato hicho huitumii kwa matumizi ya aina yoyote ile. Hii ni kwa ajili ya maisha ya baadaye, kwako wewe na vizazi vyako. 

Kama unatumia kipato chako chote unachoingiza, huwezi kutengeneza utajiri na uhuru wa kifedha, hata iweje. Tenga sehemu ya kumi na iweke pembeni. Unaitumia kufanya nini hiyo? Angalia sheria zinazofuata. 

SHERIA YA PILI YA FEDHA; FEDHA KUKUFANYIA KAZI. 

Fedha hufanya kazi kwa juhudi kwa yule mtu ambaye anaweza kuiwekeza kwenye eneo ambalo linazalisha. Kwa kifupi, fedha ni mfanyakazi mzuri, kama ukiweza kuiweka mahali pazuri na kuisimamia vizuri. 

Kile ambacho unajilipa wewe mwenyewe kwanza, siyo kwa ajili ya matumizi ya baadaye, badala yake ni kwa ajili ya kujizalishia zaidi baadaye. Ila hapa sasa fedha inakuwa inafanya kazi zaidi ya unavyofanya wewe. Hivyo unaweza kuweka fedha hiyo kwenye biashara au hata uwekezaji, kiasi kwamba itakuzalishia faida zaidi. 

SHERIA YA TATU YA FEDHA; UWEKEZAJI MAKINI. 

Fedha hung’ang’ana kwa yule ambaye anaiwekeza kwa ushauri wa watu wenye hekima. 

Ni muhimu uwekeze fedha yako kwa ushauri wa wale ambao wanajua kuhusiana na uwekezaji ambao unaufanya. Au uchukue muda kujifunza ili uwe na uhakika wa usalama wa fedha yako. 

Fedha inapowekezwa kwa umakini na ushauri wa watu wenye hekima, huzaliana zaidi na zaidi na hapo ndipo utajiri na uhuru wa kifedha unapotengenezwa. 

Rafiki yangu, hii ni sehemu ya masomo ya semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, semina ambayo nimeiendesha wiki mbili zilizopita kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA. Washiriki wote wa semina hii wameeleza kufunguliwa sana na maarifa haya. 

Kwa sababu hiyo, nimeshawishika kurudia semina hii kwa wale alioikosa. 

Hivyo leo semina hii inaanza tena kwa mara ya pili. Mwisho wa kujiunga na semina hii ilikuwa jana jumamosi. Hivyo kama mpaka sasa hujajiunga, umeshachelewa. 

Lakini kwa kuwa mimi ni rafiki yako, na kusudi langu kwenye maisha ni kuhakikisha wewe unapata maarifa sahihi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi, hasa kwenye fedha, ninaweza kukupa nafasi chache sana zilizobaki, ili na wewe usikose maarifa haya. 

Hivyo cha kufanya, ni sasa hivi, ulivyosoma huu ujumbe hapa, nitumie mesej kwenye namba 0717 396 253 mesej iwe kwa njia ya wasap. Ukishatuma ujumbe, nitaangalia uwepo wa nafasi na nitakupa maelekezo ya kujiunga. Fanya hivyo sasa, kwa sababu nafasi ni chache, na hii ninayotoa ni kwa upendeleo pekee. 

Sheria mbili za fedha zilizobaki utajifunza kwenye semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, na tutajenga msingi imara kifedha kwa kutumia sheria hizo tano na maarifa mengine muhimu. 

Huna sababu ya kukosa semina hii, labda kama wewe mwenyewe umeamua kwamba unataka kuwa masikini na kubeba changamoto za kifedha maisha yako yote. Kwa maamuzi hayo, hakuna awezaye kukupinga. 

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi