Man Utd wakamilisha kumnunua Nemanja Matic kutoka Chelsea
Manchester United wamekamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kutoka kwa mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea kwa £40m.
Mchezaji huyo ametia saini mkataba wa miaka mitatu.
Matic, 28, amekuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na United majira haya ya joto.
United walikuwa wamemnunua beki Victor Lindelof kwa £31m kutoka Benfica na kisha wakalipa £75m kumchukua Romelu Lukaku kutoka Everton.
Meneja wa United Jose Mourinho alimweleza Matic kama mchezaji anayecheza vyema na wenzake kwenye timu na "ana kila kitu ambacho tungetaka katika mwanakandanda; uaminifu, uendelevu na kuwa na ndoto kuu".
Matic amesema ana furaha sana kujiunga na United wakati huu wa kusisimua.
Mourinho, alipokuwa Chelsea, alitumia £21m kumnunua Matic kutoka Benfica kwa kipindi cha pili Stamford Bridge Januari 2014.
Thamani yake ilikuwa imekadiriwa kuwa chini ya £5m alipoihama klabu hiyo kama kikolezo wakati wa ununuzi wa David Luiz Januari 2011, miaka miwili baada yake kujiunga na Blues kwa mara ya kwanza kwa £1.5m kutoka kwa klabu ya MFK Kosice ya Slovakia.
Matic alifunga bao moja katika mechi 35 alizochezea Chelsea Ligi ya Premia msimu wa 2016-17, ambapo pia alifunga bao la kipekee wakati wa ushindi wao nusufainali Kombe la FA dhidi ya Tottenham Aprili.
Chanzo:BBC
Comments
Post a Comment