Trump alimfunza mwanawe maneno ya kusema mkutanoni
Rais Donald Trump alimfunza mwanawe maneno aliyofaa kusema kuhusu mkutano na wakili wa Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi , kulingana na ripoti ya vyombo vya habari.
Taarifa hio ilisema Donald Trump Jr na wakili huyo kwanza walizungumza kuhusu upangaji wa watoto nchini Urusi mnamo mwezi Juni 2016 kulingana na gazeti la Washington Post.
Bwana Trump Jr baadaye alisema kuwa amekubali kushiriki katika mkutano huo baada ya kuambiwa kwamba angepewa habari ya kumchafulia jina Hillary Clinton.
Rais Trump amekana ushirikiano wowote na Urusi wakati wa kampeni.
Bunge la seneti , lile la wawakilishi na mtaalam mmoja wanachunguza uingiliaji huo wa Urusi katika uchaguzi mkuu swala linalopingwa na Urusi.
Gazeti la The Washington Post kwanza liliripoti kwamba rais Trump yeye mwenyewe alimfunza taarifa ambayo mwanawe alitoa kuhusu mkutano na wakili Natalia Veselnitskaya.
Gazeti hilo lilitaja duru kadhaa ambazo zilitambua mazungumzo hayo.
Washauri wa rais Trump walikubali kwamba mwana huyo atatoa taarifa ya ukweli ambayo isingiweza kukanushwa baadaye iwapo maelezo yote yangebainika ,kulingana na Washington Post.
Lakini inasema kuwa uamuzi huo ulibatilishwa baada ya rais Trump kuelekea nyumbani kutoka kikao cha G20 nchini Ujerumani mnamo mwezi Julai 8.
Katika taarifa hiyo , bwana Trump Jr alisema kuwa mkutano huo ulijadili kuhusu mpango kuhusu upangaji wa watoto wa Urusi, na sio maswala ya kampeni.
Taarifa hiyo iliwasilishwa katika gazeti la The New York Times wakati ilipokuwa likitayarisha habari yake kuhusu mkutano huo.
Bwana Trump Jr baadaye alikiri kwamba alikubali kukutana baada ya kuambiwa kwamba habari mbaya kuhusu Clinton pia zitatolewa katika mkutano huo.
Pia alitoa barua pepe ambazo zilikuwa chanzo cha mkutano huo .
Washington post linasema kuwa baadhi ya washauri wa rais Trump wanahofu kwamba kiwango cha uingiliaji huo uliofanywa na rais kinaweza kumtia mashakani kisheria.
Trump na mwanawe hawajatoa tamko lolote kuhusu ripoti hizo za vyombo vya habari.
chanzo:BBC SWAHILI
Comments
Post a Comment