Kimbunga Irma chakaribia Florida
Nguvu ya upepo mkali unaondamana na kimbunga, kimeanza kugonga visiwa kadhaa kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani, huku kimbunga kikiacha uharibifu mkubwa katika visiwa vilivyoko kwenye bahari ya Atlantic huko Caribbean, kuelekea Marekani.
Kimbunga Irma, kinatarajiwa kugonga maeneo hayo, baadaye leo Jumapili.
Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajia kimbunga kikubwa kuwasili.
Taharuki na hatma ya baadaye ya mji wa Tampa, ambao unakabiliana ana kwa ana na njia inakopitia kimbunga hicho, haijulikani.
Tampa inasemekana kuwa ni mji ulioko katika mazingira magumu zaidi nchini Marekani, hasa kuhusiana na hatari ya kugongwa mara kwa mara na vimbunga.
Zaidi ya watu milioni 6 huko Florida wanaondolewa majumbani mwao- robo tatu ya idadi nzima ya watu wa jimbo hilo.
Wakuu katika jimbo hilo wametangaza hali ya tahadhari ya kutotoka nje, katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo, ukiwemo mji wa Miami.
Comments
Post a Comment