Wapiganaji wa Rohingya watangaza kusitisha mapigano, Myanmar

Wa Rohingya wanaishutumu jeshi la Myanmar kwa kuteketeza vijiji vyao - Lakini utawala nchini Myanmar, unasema wanajeshi wake wanakabiliana na "magaidi"


Haki miliki ya pichaEPA
Image captionWa Rohingya wanaishutumu jeshi la Myanmar kwa kuteketeza vijiji vyao - Lakini utawala nchini Myanmar, unasema wanajeshi wake wanakabiliana na "magaidi"

Katika taarifa nyingine Asubuhi hii ya leo, waasi wa kiislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wametangaza upande mmoja makubaliano ya kusitisha mapigano leo Jumapili, ili kujaribu kupunguza mgogoro wa kibinadamu magharibi mwa taifa hilo.
Mashambulio dhidi ya jeshi la taifa hilo yanayotekelezwa wapiganaji wa Arakan Rohingya Salvation Army, yalisababisha mapigano makali ya wiki mbili, ambapo zaidi ya watu laki tatu wa jamii ndogo ya Warohingya wamekimbilia nchi jirani la Bangladesh. 

Ramani ya Myanmar
Image captionRamani ya Myanmar

Kundi hilo la waasi, yameiomba jeshi la nchi hiyo pia kuitisha wito wa kusitisha mapigano, huku likiomba mashirika ya utoaaji misaada ya kibinadamu kurejelea kazi zao za kusambaza misaada.
Waziri mmoja wa serikali ya Myanmar ameiambia BBC kuwa, wengi wa Wa-Rohingya waliokimbia nchi hiyo na kuelekea Bangladesh, hawataruhusiwa kamwe kurejea Myanmar.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi