Rais Trump Anasema Taasisi ya Umoja Wa Mataifa Haifanyi Vizuri
Rais wa Marekani Donald Trump alifungua mzunguko wa majadiliano ya pamoja Jumatatu mwanzoni mwa vikao vya kidiplomasia vya siku nne huko New York nchini Marekani kwa ajili ya kikao cha mwaka cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa na mikutano mingine ya pembeni.
Akionekana kwa mara ya kwanza kwenye Umoja wa Mataifa hiyo Jumatatu siku moja kabla ya kufunguliwa rasmi kwa kikao cha baraza kuu Rais Trump aliongoza kikao kuhusu mageuzi katika taasisi hiyo ya dunia na kutaka hatua za kijasiri zichukuliwe kuifanya taasisi hiyo yenye mataifa wanachama 193 iwe taasisi yenye nguvu kwa amani.
Akizungumza pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres na balozi wa Washington katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, Rais Trump aliwaambia wanadiplomasia kwenye mkutano wa mageuzi kwamba taasisi hiyo haifanyi vizuri kama inavyotakiwa na kwamba urasimu ndio wa kulaumiwa. Alisema viongozi wa dunia lazima wasizuiwe katika kutumia njia za zamani.
Comments
Post a Comment