Rooney ahukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili
Nahodha wa zamani watimu ya taifa ya England Wayne Rooney amehukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili sambamba na kufanya kazi za jamii kwa saa 100.
Rooney 31, alikamatwa kwenye kitongoji cha Wilmslow, Cheshire kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa Septemba 1.
Rooney pia atalipa faini ya Pauni 170 kwa kosa hilo.
''Nimekubali kosa langu na nimeomba radhi kwa familia, klabu yangu ya Everton, mwalimu na sasa ni zamu ya mashabiki.Ninaomba radhi kwa kitendo kile.'' alisema Rooney baba wa watoto watatu.
Mchezaji huyo aliyezaliwa katika jiji la Liverpool alijiunga na Everton klabu yake ya utotoni akitokea Manchester United miaka 13 baada ya kuondoka.
Comments
Post a Comment