Uchaguzi wa Rai Kenya huenda ukasogezwa mbele


Uchaguzi mpya wa urais nchini Kenya huenda ukaahirishwa kutoka tarehe 17 mwezi ujao. Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imekuwa ikikutana kuangalia uwezekano wa kuahirisha Uchaguzi huu baada ya kampuni ya Ufaransa ya Safran Morpho kuomba muda zaidi kuboresha mitambo inayotumiwa kuwatambua wapiga kura.

Mbali na hilo, Muungano wa Upinzani Nasa, unaoongozwa na Raila Odinga, umesema Uchaguzi hautafanyika iwapo marekebisho hayatafanyika ndani ya Tume ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Ezra Chiloba Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.

Chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kinashutumu shinikizo hilo la upinzani na kusisitiza uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi