Posts

Showing posts from November, 2017

Arsenal yaichapa Huddersfield Town 5-0

Image
Image caption Arsenal kwa sasa ipo nafasi ya nne na alama 28 Arsenal imeweza kutakata vilivyo ikiwa nyumbani baada ya kuichapa Huddersfield Town 5-0 katika mchezo ambao Arsenal ilitawala kila idara. Magoli ya Arsenal yamepachikwa na Alexandre Lacazette, Olivier Giroud akiingia nyavuni mara mbili, Alexis Sánchez na Mesut Özil. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema ni faraja kupata alama tatu muhimu hususan wakati huu ambapo timu zinacheza michezo mingi. Kwa upande wa David Wagner anayekinoa kikosi cha Huddersfield ametaja matokeo hayo kuwa mabaya na kuongeza kuwa ligi ya EPL ni ngumu kwani kila timu ina uwezo wa kushinda. Kwa matokeo hayo Arsenal inapanda mpaka nafasi ya nne ikiwa na alama 28.

Marekani yaitaka dunia kusitisha biashara na Korea Kaskazini

Image
Image caption Kombora hili linasemekana kuwa na uwezo wa kufika sehemu yoyote ya Marekani Marekani imetoa wito kwa mataifa mbalimbai kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na kibiashara na Korea Kaskazini, ikiwa ni hatua ya kupinga majaribio ya makombora ambayo yamekuwa yakifanywa na taifa hilo. Balozi wa Marekani Nikki Haley, ametoa pendekezo hilo katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa unaoendelea mjini New York. Bi. Haley amesema kuwa Rais wa Marekani amemtaka Rais wa China Xi Jinping kusitisha biashara ya mafuta ghafi na Korea Kaskazini, kama sehemu ya kutekeleza hatua ya kuwekewa vikwazo kwa taifa hilo. Korea Kaskazini: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani Kupitia hatua hii ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini tunapaswa kusitisha asilimia tisini ya biashara na Korea Kaskazini pamoja na asilimia 30 yamafuta yake. Msambazaji mkubwa wa mafuta Korea Kaskazini ni China. Image caption Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Mwaka 2003, Ch...

Praljak: Mhalifu wa kivita afariki baada ya kunywa sumu mahakamani The Hague

Image
Haki miliki ya picha ICTY Kikao cha kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita mjini The Hague, Uholanzi kimesitishwa ghafla baada ya mmoja wa washtakiwa kusema amekunywa sumu baada ya kusikiliza hukumu. Slobodan Praljak, 72, alikuwa mmoja wa viongozi sita wa zamani wa kisiasa na wa kijeshi wa Bosnia wa asili ya Croatia ambao walikuwa wamefika mahakamani. Amefariki akitibiwa hospitalini na Umoja wa Mataifa umesema sasa mahakama hiyo ni "eneo la uhalifu". Alikuwa amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 mnamo 2013 kwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika mji wa Mostar. Baada ya kusikiliza hukumu kwamba majaji walikuwa wamedumisha kifungo hicho, alimwambia jaji, "Nimekunywa sumu". Sita hao walikuwa wanasikiliza uamuzi wa mwisho wa rufaa uliokuwa unatolewa na mahakama maalum ya kimataifa ya UN iliyokuwa inashughulikiwa makosa yaliyotekelezwa Yugoslavia (ICTY). Ingawa walikuwa washirika dhidi ya Waserbia wa Bosnia wakat...

Rais Trump amshutumu waziri mkuu wa Uingereza Theresa May

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Rais Trump na waziri mkuu nchini Uingereza Theresa May Rais Donald Trump amemwambia waziri mkuu wa Uingereza Theresa May kuangazia ugaidi nchini Uingereza badala ya kumkosoa kwa kusambaza video za kundi la mrengo wa kulia la Uingereza ambalo linaeneza chuki. ''Usiniangazie sana mimi, angazia ugaidi unaotekelezwa na makundi yalio na itikadi kali ambao unatekelezwa nchini humo'', Trump alituma ujumbe wa Twitter. Rais huyo wa Marekani awali alituma video tatu zenye chuki zilizosambazwa katika mtandao wa Twitter na makundi hayo nchini Uingereza. Msemaji wa bi May alisema kuwa ni makosa kwa rais kufanya hivyo. Marekani na Uingereza ni washirika wa karibu na wameelezewa kuwa na ''uhusiano maalum''. Theresa May alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kumtembelea rais Trump katika ikulu ya Whitehouse. Haki miliki ya picha TWITTER Image caption Ujumbe wa twitter uliotumwa na rais Trump Kanda za vide...

Marekani yataka mataifa yote kukatiza uhusiano na Korea Kaskazini

Image
Image caption Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un na mwenzake wa Marekani Donald Trump Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu. Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa Pyongyang. Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka. Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili. Korea Kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani. Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo. Hatahivyo kiongozi wa...

Tyson Fury: Nitataka kupigana na mtu mwenye jina kubwa zaidi

Image
Image caption Fury baada ya kumchapa Wladimir Klitschko mwaka 2015 Bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani Tyson Fury amesema atapenda kupigana na mtu mwenye jina kubwa iwapo atarejea uwajani. Fury mwenye miaka 29 tiyari ameshasaini mkataba na kampuni ya MTK akijiandaa kumaliza adhabu yake. Anatarajia kusikia uamuzi wa mahakama mwezi Desemba dhidi ya kesi yake ya matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni mwaka 2016. ''Naweza kuitwa mkorofi, mgomvi na mambo mengine ya aina hiyo, lakini sio mtumizi wa dawa za kuongeza nguvu,'' alisema Fury raia wa Uingereza. Chama cha ndondi nchini Uingereza kimesema bingwa huyo ambaye alipata mikanda ya IBF, WBA na WBO kwa kumchapa Wladimir Klitschko Novemba 2015, hatopewa leseni ya kupigana mpaka pale mambo yote yatakapowekwa sawa.

Manchester United yaichapa Watford 4-2

Image
Image caption Ashley Young alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo Manchester United ikiwa ugenini katika dimba la Vicarage Road imefanikiwa kuichapa Watford 4-2 katika ushindi ambao awali ulionekana kuwa mgumu kwa United kabla ya kuanza kwa mchezo. Magoli ya United yamefungwa na Ashley Young akiingia nyavuni mara mbili huku Antony Martial akipachika goli la tatu na Jesse Lingard. Troy Deeney na Doucaure walindika magoli mawili ya Watford. Meneja wa Manchester United José Mourinho amesema ushindi huo utaongezaotisha kwa timu yake. Image caption Wachezaji wa Watford wakishangilia Man United inasalia nafasi ya pili ikiwa na alama 32 ikiwa ni alama tano nyuma ya Man City ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi.

Uchaguzi Kenya: Kenyatta aapishwa na kuahidi kuliunganisha taifa

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Kenyatta ameapishwa kuongoza kwa muhula wa pili na wa mwisho Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameahidi kuunganisha taifa hilo katika muhula wake wa pili uongozini baada ya kuapishwa katika sherehe ambayo ilisusiwa na viongozi wa upinzani. Akihutubu baada ya kula kiapo uwanjani Kasarani, Nairobi kiongozi huyo alisema ameyasikia baadhi ya mapendekezo ya upinzani na atazingatia baadhi. Hata hivyo aliwahimiza viongozi wa upinzani kuheshimu sheria na katiba ya nchi hiyo. Muungano wa upinzani, ambao ulisusia uchaguzi wa marudio tarehe 26 Oktoba, ulikuwa umepanga mkutano wa hadhara kuombolewa wafuasi wa muungano huo ambao wameuawa katika makabiliano na maafisa wa polisi. Mkutano huo haukufanyika kama ulivyopangwa katika uwanja wa Jacaranda, lakini kiongozi wa National Super Alliance Raila Odinga akihutubia wafuasi wake karibu na uwanja huo alitangaza mpango wa kumuapisha kuwa rais mwezi ujao tarehe 12, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Jamhur...