Manchester United yaichapa Watford 4-2
Manchester United ikiwa ugenini katika dimba la Vicarage Road imefanikiwa kuichapa Watford 4-2 katika ushindi ambao awali ulionekana kuwa mgumu kwa United kabla ya kuanza kwa mchezo.
Magoli ya United yamefungwa na Ashley Young akiingia nyavuni mara mbili huku Antony Martial akipachika goli la tatu na Jesse Lingard.
Troy Deeney na Doucaure walindika magoli mawili ya Watford.
Meneja wa Manchester United José Mourinho amesema ushindi huo utaongezaotisha kwa timu yake.
Man United inasalia nafasi ya pili ikiwa na alama 32 ikiwa ni alama tano nyuma ya Man City ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi.
Comments
Post a Comment